CCM DODOMA yapata VIONGOZI WAPYA, MWENYEKITI MPYA ADAM KIMBISA
BONGONEWZ BLOG
Ndugu Kimbisa amepata nafasi hiyo baada ya kupata kura 941 Kati ya kura 1196 zilizopigwa huku mbili zikiharibika.
Katika nafasi hiyo aligombea na wenzake watatu ambao ni mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma ndugu William Kusila aliyepata kura 216 na mwenyekiti mstaafu wa wilaya ya Dodoma mjini ndugu Denis Bendera aliyepata kura 30.
Akizungumza
mara baada ya matokeo kutangazwa ndugu Kimbisa amewataka wanachama
kuvunja makundi yaliyokuwepo wakati wa kampeni ili kwa pamoja waweze
kujenga chama.
Amewataka wanaodhani hivyo kuelewa kuwa CCM sio chama cha kukimbilia Pindi watu wakitaka uongozi.
Mkoa wa Dodoma umepata mwenyekiti mpya ndugu Adam Kimbisa atakaye kiongoza Chama kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Katika nafasi hiyo aligombea na wenzake watatu ambao ni mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma ndugu William Kusila aliyepata kura 216 na mwenyekiti mstaafu wa wilaya ya Dodoma mjini ndugu Denis Bendera aliyepata kura 30.
Awali
akifungua mkutano huo wa uchaguzi Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr Rehema
Nchimbi ambaye ndie aliyekuwa msimamizi mkuu aliwataka wananchi kuelewa
kuwa CCM sio ngazi ya kupanda ili mtu apate uongozi kama ambavyo wengine
wanadhani.
Leo
kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kinaketi kwa ajili ya kuchagua Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Mkoa na Katibu wa Fedha na Uchumi.
Ambapo
mpaka sasa matokeo yamekuwa ni katibu itikadi na uenezi wa mkoa
amechaguliwa Donald Mejiti na katibu wa uchumi na fedha amechaguliwa
Mohamedi Rashid Morama.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII