HIKI NDICHO ALICHOTAMKA MJANE WA MWANGOSI BAADA YA VYOMBO VYA HABARI KUDAI KUWA ANAMSHUTUMU DR.SLAA..

Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi amekanusha vikali habari zilizochapishwa na gazeti la habari Leo kuwa eti yeye alimshutumu Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa kuhusu rambirambi za mumewe.Akiongea na Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amesema kwa uchungu mkubwa kuwa amesikitishwa sana kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na ni aibu kubwa chombo kikubwa cha habari kama Habari Leo kutoa habari ya uongo kwa viwango hivyo. Mjane huyo amesema kama angekuwa na Shida na Dr Slaa angemtafuta mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CDM na kwa hapa Iringa yeye na Msigwa ni majirani. Mjane huyo ameendelea kusema kitendo hicho kilichofanywa na gazeti hilo kimeamsha Msiba upya kwake kwani kina lengo la kutaka Jamii imdharau. Anaomba watanzania kuupuza habari hizo na ameshanga ni maadili gani haya ya uandishi na hajui kwa hali hii Taifa linakwenda wapi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

1 comment:

  1. Too bad. Serikali isipoacha ujinga wake sijui itaishia wapi.

    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs