HIVI NDO VIJEMBE VYA KIGWANGALA ALIVYOANDIKA FB BAADA YA KUMGARAGAZA BASHE IGUNGA

BongoNewz
Ikiwa inasemekana kuwa ni dongo kwa hasimu wake mkubwa katika siasa za CCM, Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangala ameandika ujumbe ufuatao Facebook.....nsikuchoshe sana, endelea kusoma hapa...
 "Uchaguzi Mkuu wa CCM Wilaya ya Nzega umemalizika salama na tumepata viongozi mahiri. Ni imani yangu tukiwapa ushirikiano wa kutosha CCM sasa itakuwa moja, imara na yenye kusonga mbele. Hongereni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Nzega kwa kung'oa kwa kiasi kikubwa vigogo na waasisi wa siasa za ufuasi na wenye kufanya siasa za kumridhisha mtu mmoja tu, pia kwa kuwakwamisha wengi wa wafuasi wa siasa hizo na kuingiza majembe ya ukweli! Mmedhihirisha pesa peke yake si kigezo cha kushinda uchaguzi, mmefanya kweli. Nawashukuruni nyote kwa kufuata na kutumia ushauri wangu kwamba tujenge CCM moja imara, kusiwe na watu wa Kigwangalla na wala wa Selelii, kuwe na wanaCCM wamoja...mlinipa faraja ya ushindi na pale mliponibeba juu juu niliogopa kwamba msije mkawa mmedhamiria kwenda kunitupa, ila nakushukuruni sana hamkufanya hivyo badala yake mlishukuru kwa ushauri wangu..."

"Mara baada ya fununu za matokeo ya uchaguzi kuwa wazi kuna watu wawili maarufu walizimia, na walipozinduka waliangua vilio na hawajaonekana Nzega tena...tunawapa pole na kuwatakia quick recovery huko waliko! Huo ndiyo ushindani...na sisi tunawaambia kuwa wasihofu kitu watatendewa haki siku zote katika chama hiki na katika uongozi huu. Malengo yetu ilikuwa ni kuondoa watu wa hovyo, wachumia tumbo na wanaofanya kazi kwa maelekezo ya mtu mmoja tu na sasa kuweka watu makini na mahiri watakaokisimamisha chama, hata kama itamaanisha kuniadhibu mimi pale itakapobidi...Chama Kwanza, Mtu baadaye! Hakuna mtu maarufu na wa maana ndani ya CCM kuliko CCM yenyewe. Nimesikia wanataka kuikimbia nchi, tunawasihi wasifanye hivyo, waendelee tu kuwa waadilifu na waaminifu kwa chama na kwa nchi na ipo siku mambo yao yatawanyookea tu!"
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs