LHRC yaishtaki serikali ya Tanzania ICC

Katika hali inayoleta matumaini kituo cha haki na sheria kimeishaki serikali katika mahakama ya ICC.Akizungumzia hatua hiyo bibi helen kijo,alisema hatua hiyo ni ya mwanzo na hawatarudi nyuma hivyo kuwaomba watanzania kuwaunga mkon
Bibi kijo amesema kuwa wameiomba mahakama hiyo kufanya uchunguzi wa mauwaji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na serikali kupitia jeshi la polisi na kusema wamefungua pia shauri kama hilo katika mahakama ya africa.

Amesema kitendo cha serikali kuwahamisha watendaji wanaofanya mauwaji hayo na kuwapeleka sehemu nyingine bila kuwawajibisha hakivumiliki na kuwa hawata kaakinya mpaka watendaji hao watakapo wajibishwa na sheria kufata mkondo wake.

Huku akitolea mfano wa kamanda wa mkoa wa iringa aliye hamishiwa iringa kwa kosa la mauwaji
na kurudia kitendo kilekile cha kuwauwa raia wasio na hatia na mpaka sasa hajachukuliwa hatua yoyote,huku serikali kupitia waziri wa mambo ya ndani kwa kitumia kodi za walalahoi wakijaribu kuficha ushahidi.

Bibi kijo amesema ni lazima serikali iwawajibishe wote waliohusika na mauwaji ya watanzania na kusema si iringa pekee,ni pamoja na mikoa yote ambayo mauwaji kama hayo yalipotokea.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs