HII NDO ALICHOKISEMA SAJUKI, KUHUSU KUDONDOKA JUKWAANI
Ni kweli ninaumwa sana, lakini ninapojiona nina nguvu kidogo lazima nihangaike maana sina duka linaloingiza pesa kwa ajili ya matumizi ya familia yangu, sina mama anayenipa fedha au msaada," alisema.
Sajuki anasema kuwa pamoja na kuumwa, lakini haikuwa rahisi kurudi katika vyombo vya habari tena kwa ajili ya kuwaomba Watanzania wamchangie fedha kwa sababu kurudi India kwa ajili ya matibabu awamu ya pili baada ya muda wa kurudi kufika.
Msanii huyo anasumbuliwa na saratani ya ngozi na mgongo maradhi yaliyogundulika alivyokuwa India.
Kwa maradhi hayo anatakiwa kupumzika muda mwingi na kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa madaktari akisubiri safari ya kwenda India kwa matibabu zaidi.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII