RIHANNA ASEMA ATAMUUA CHRIS BROWN ENDAPO ATAMUACHA
MWANAMUZIKI Rihanna ambaye ndio kwanza amerudiana na Chris Brown, amesema kamwe hawezi kukubali kuachana na mwanamume huyo na ameenda mbali kwa kusema kama watalazimika kuachana, mmoja wao atakufa.
Rihanna amesema kuwa yupo tayari kumuua mpenzi wake huyo ili asahau kama kuna mtu kama huyo ambaye aliwahi kumpenda.
Rafiki wa karibu wa Rihanna alisema: "Rihanna amemwambia wazi Chris kwamba hawezi kumwacha wala kuvumilia kuona akiwa na mpenzi mwingine, hivyo yupo tayari kumuua kama akijaribu kufanya hivyo.
"Alikuwa na wakati mgumu kwa muda mrefu. Aliamua kumrudia mwanamume huyo kwa sababu anampenda kwa dhati. Haoni kama maisha yana thamani bila ya mwanaume huyo.
"Lakini mpango wa Rihanna wa kumuua Chris huenda usifanikiwe kwa kuwa mwanaume huyo amewaambia rafiki zake kuwa anataka kufunga ndoa na dada huyo na kamwe hawezi kumwacha."
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII