SHAMSA FORD: NAOMBA JAMII ITUSAMEHE KUHUSU KASHFA YA NGONO
MWIGIZAJI wa kike wa filamu Bongo Shamsa Ford amewaomba wapenzi wa
filamu wawapokee wasanii wa kundi la Bongo Movie unity baada
ya kuundwa upya kufuatia kubadilisha uongozi uliopita kushindwa kulinda
nidhamu na maadili ya Mtanzania na kukumbwa na kashifa za ngono na
kuteka vyombo vya habari kwa habari mbaya tu.
“Ni kweli kuna wenzetu ambao wametuchafua kweli kutokana na mambo yao
ya ajabu, lakini sisi tunaojielewa tunaomba jamii itupokee kama wasanii
wao tunaowategemea wao kama mashabiki wetu na tunawahitaji sisi ni sawa
na mtoto akichafuka mkono hauwezi kukatwa, tunahitaji kusamehewa kutokana
na watu wachache wasio na maadili mema’”anasema Shamsa.
Msanii huyo ambaye amekiri kwa kusema kuwa kundi hilo kwa sasa limechafuka katika jamii ni kutokana na tabia mbaya za wasanii wachache ambao inawezekana nyuma ya pazia kuna biashara nyingine wanayotegemea ndio maana wanafanya upuuzi unaowatukanisha wanawake waliopo katika tasnia ya filamu na jamii kuwapuuzia kama ni watu wasiojitambua.

0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII