WASTARA AWAOMBA WATANZANIA WASIMLAUMU KUHUSU KIFO CHA MUMEWE SAJUKI

STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, aliyekuwa mke wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, amewaomba Watanzania wakiwemo wasanii wenzake kuacha kuongea mambo mengi kwenye magazeti ikiwa ni pamoja na lawama na kwamba dua kwa marehemu ndiyo jambo la msingi kwa sasa.
Wastara Juma.
Akizungumza na Gazeti la Ijumaa hivi karibuni, Wastara alisema watu wanaongea mengi na wataongea mengi kuhusu marehemu mume wake ikiwa ni pamoja na lawama za nani amesababisha kifo, nani hajasababisha lakini akasema waachane kabisa na mambo hayo kwani aliyeumia sana ni yeye.
“Ukweli utabaki kuwa Sajuki ameondoka kwa mipango ya Mungu, tuache lawama zisizo na msingi, tumuombee mwenzetu huko aliko apumzike kwa amani lakini waniombee pia niweze kuvuka kipindi hiki kigumu,” alisema Wastara.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs