PICHA ZA UZINDUZI WA KILI MUSIC AWARDS ULIOFANYIKA LEO ..ZITAZAME HAPA
Baraza
la sanaa la Taifa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo wamezindua
rasmi tuzo za muziki za Tanzania zijulikanazo zaidi kama Kili Music
Awards.
Katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam bia ya
Kilimanjaro ambayo ndio wadhamini wakuu wa tuzo hizo wamesaini mkataba
wa miaka mitano na BASATA wa kuzidhamini ambapo zaidi ya shilingi
bilioni 4 zitatumika kuziandaa kwa kipindi hicho.
Tuzo za mwaka huu zitafanyika tarehe 8 June kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
“Lengo hasa la kusaani mkataba huu ni kuwahakikisha watanzania kuwa
tutaendelea kuwapa tuzo hizi na tutaendelea kuzifanya kwa kusikiliza
matakwa ya wadau wa sanaa ya muziki Tanzania wanataka nini ili sisi kama
wadhamini kuhakikisha wanakipata kile wanachokitaka,” alisema Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe.
Kavishe amesema tuzo za Kilimanjaro ni miongoni mwa tuzo kubwa kabisa za muziki barani Afrika.
“Wale wanaofuatilia tuzo za muziki Tanzania, barani Afrika na duniani
kwa ujumla mtakubaliana na mimi kabisa kwamba tuzo hizi kwa hapa
Tanzania na kwa Afrika kwa ujumla ni za ukubwa kuliko tuzo zote
zinazotolewa, ilikuwa inatanguliwa na Kora Music, MTV na Channel O
awards.”
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa BASATA, Godfrey L. Mngereza
alisema juhudi za BASATA na wadhamini wa tuzo hizo, zimeifanya serikali
iitambue rasmi tasnia ya muziki kama shughuli rasmi. “Kwahiyo tasnia ya
muziki ni rasmi kuanzia January mwaka huu,” alisema Mngereza.
“Baraza linachukua fursa hii kuwaasa wasanii kuthamini program hii na
kuongeza ubunifu wa kazi zao ili ziwe katika viwango vya kitaifa na
kimataifa.”
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII