ARSENAL, CHELSEA HAKUNA MBABE, LIVERPOOL BADO IKO JUU

Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud (kulia) akipiga mpira mbele ya beki wa Chelsea, Gary Cahill.
Frank Lampard wa Chelsea (kushoto) akikwaana na Mesut Ozil wa Arsenal wakati wa mchezo wa leo uliomalizika 0-0.
Mchezaji wa Chelsea, Eden Hazard, akijaribu kumtoka kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey (kulia). Kati ni Theo Walcott.
 Frank Lampard wa Chelsea akiwa chini na beki wa Arsenal, Bacary Sagna (juu) wakati wa patashika ya mechi ya leo.
Timu za Arsenal na Chelsea zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England iliyopigwa Uwanja wa Emirates jijini London hivi punde!
Kwa matokeo ya leo Arsenal wamefikisha pointi 36 sawa na Liverpool lakini wakiwa nafasi ya pili. Liverpool wao wanaongoza kwa tofauti ya mabao 23 huku Arsenal wakiwa na 16.
Manchester City wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 35 huku Chelsea wakiwa nafasi ya nne kwa pointi 34 sawa na Everton waliopo nafasi ya tano.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs