BINTI AJITOKEZA NA KUDAI KUWA NDIO ALIZAMISHA MELI YA MV SPICE ISLANDERS.....SOMA HAPA

Ikiwa Ni Miaka Miwili Tangu Tupoteze Ndg, Jamaa & Marafiki Ktk Ajali Ya Kuzama Kwa Meli Ya Mv Spiee Islander Ameibuka Bint Mmoja Anayeitwa Theresia Na Kudai Ndiye Aliyeizamisha Meli Ya Islander Kichawi Usiku Wa Tarehe 9/9/2011 Katika Mkondo Wa Nungwi Ikiwa Ni Kutii Agizo La 'wakubwa' Katika Zoezi La Kukusanya Damu Kwa Matumizi Ya Kichawi.

Theresia Ameeleza Hayo Wakati Akitoa Ushuda Mbele Ya Mch Gwajima Katika Viwanja Vya Tangamano Jijini Tanga... Theresia Ameendelea Kumwaga Siri Kwa Kusema Alichukuliwa Kichawi Na Kupelekwa Katikati Ya Bahari Ya Pacific Na Kuishi Miaka Saba Akifundishwa Uchawi Huku Mama Yake Asijue Lolote Kwa Kuachiwa Toy Alilojua Mwanaye Kwa Kipindi Chote Hicho.

Theresia Huku Akiongea Na Maneno Kadha Ya Kingereza (english) Safi Aliendelea Kudai siku Ya Tukio Alitumwa Na 'Wakubwa' Akiongoza Kikosi Cha Watu 4 Yeye Wa5 Walifanikiwa Kuivutia Chini Ya Maji Meli Hali Iliyosababisha Vifo Vingi Na Kurahisisha Zoezi La Kukusanya Damu Hiyo.




Theresia akieleza ushuhuda kamili huku mama yake pembeni akisikiliza.
Siku moja nilikuwa nimetumwa na mama yangu mkubwa, wakati navuka barabara ghafula nikakutana na mtu ana kila kitu kimoja , akajitambulisha kwa jina la Lucifer akanipa mkono ila nikakataa, akauchukua mkono wangu kwa nguvu akanikumbatia, nikajikuta chini ya bahari. Akaja mwenyewe nikaogopa sana akaniambia nimekuchagua kwa sababu nimekuchagua hata kabla hujazaliwa. Kwa sababu una akili sana.

Akaniambia nilipozaliwa aliniwinda sana ila alishindwa kunichukua kwa sababu bibi yangu alikuwa ananiombea sana . Lucifer kaniambia anataka niwe mke wa mtoto wake. Tukafunga ndoa na baada ya miezi 6 baba yake akaniambia anaweza kunipa nguvu nyingi sana lakini anataka nimtumikie yeye. Baada ya miaka 6 akanipeleka sehemu Fulani ndani ya bahari ya pacific lakini ni chini sana, sehemu hiyo ni mji kama ilivyo miji ya huku.

Tukaingia sehemu Fulani tukamkuta dragon ambae alianza kuongea na Lucifer, nikafunga macho na nikajisikia kujawa na nguvu sana, akaniambia amenipa nguvu na mamlaka ya kumiliki na kutawala fahamu za watu.

Siku moja niliamka asubuhi nikiwa na njaa sana kwa sababu usiku wake sikula chakula, Lucifer akaniambia kuna meli inaitwa Mv spice nikaenda na baadhi ya watu tukatega nyaya za copa wire ile meli ikawa inakuja tukatega pale maji yanapogawanyikia ili watu waseme ni mkondo wa maji, kuna maneno nikayasema halafu nikasimama pembeni, ile meli ikaanza kuzama mpaka kwenye kina cha chini kabisa cha bahari ambacho nilitaka mimi, kisha wale watu wakaunganisha mabomba mpaka kule nilipokuwa na tukapata damu nyingi sana. Mimi nilikuwa na uwezo wa kunywa damu kiasi cha tani 5000.

Mchungaji Josephat Gwajima akimuombea Theresia.

Pia kazi yetu nyingine ilikuwa kuwafanya watu wanaompenda Mungu waache kabisa na kuanza kuwaza vitu vilivyo tofauti kabisa na mapenzi ya Mungu.

Nakumbuka ilikuwa muda wa kulala kama kawaida nikasikia watu wanaita njooo njoooo, mara nikasikia nguvu zinaniishia na nikawa sijielewi kabisa mara nikashanga nimetokea katika viwanja vya tangamano.

Mama yake Theresia anasema kabla ya mtoto wake kurudi alikuwa na matatizo ya kuumwa magojwa yasiyoisha ya kila wakati. Pia alikuwa na tabia ya uvivu na kulala sana , pia hakupenda kusali kabisa, pia kipindi cha mitihani aliugua sana.



USHAURI ANAOTOA THERESIA KWA WATU WENGINE


Watu inabidi wamtafute Yesu kwa kiwango cha juu sana, kwa sababu yeye ndiye atakayeweza kuwapa kila kitu wanachokihitaji, pia anasema vijana wengi wapo kwenye hatari ya kuangamia hivyo kama hawatamtafuta Mungu hakika wataangamia .

Pia anamshukuru Mungu kwa kumrudisha kutoka katika vifungo vya ajabu, anachoweza kufanya ni kumtumikia Mungu na kumpenda daima. AMEN


Huo ndio ushuhuda kamili kama ulivyowakilishwa na kitengo cha huduma ya mawasiliano kanisa la Ufufuo na Uzima . Ushuhuda huu umeshuhudiwa na binti huyo wakati wa mkutano wa kiroho ulioandaliwa na kanisa hilo, na kufanyika jijini Tanga wiki iliyopita.



SOURCE;; GOSPEL KITAA.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs