MAMA KANUMBA AOMBA WADAU WAMSAIDIE


MAMA wa msanii nguli wa filamu nchini marehemu ‘Steven Kanumba’ Frola Mtegoa amesema yuko katika mkakati wa kuandaa filamu inayohusu maisha ya mwanaye kiasi cha kufikia hatua ya kuomba msaada ‘kutembeza bakuli’.
Mama mzazi wa marehemu ‘Steven Kanumba’ Frola Mtegoa.
Akizungumza na paparazi wetu mama huyo alisema kwamba, anapata wakati mgumu kukamilisha jambo hilo kutokana na kukwama na kutaka asaidiwe ili kufanikisha jambo hilo.
“Nimekwama na nawaomba wadau wajitokeze kunisaidia nikamilishe hili, nahitaji msaada wa kifedha na hata ushauri,”alisema.
Mama huyo alisema lengo la kuandaa kazi hiyo ni kutaka kufikisha ujumbe katika jamii kwa kuamini kwamba wengi watajifunza kupitia maisha ya mwanawe.
Marehemu Steven Kanumba.
Amemtaka yeyote ambaye atakayeguswa na jambo hilo asisite kuwasaliana naye na kumsaidia.

                                                                            GPL
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs