SO SAD!! MWANAMKE AMKATA MWANAUME KORODANI ZAKE HUKO SIMIYU, SOMA NA TAZAMA PICHA HAPA
JESHI
la Polisi mkoani Simiyu linamshikilia mwanamke na mkazi wa Kijiji cha
Usiulize wilayani Meatu kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake kwa kumvuta
korodani, kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo alisema tukio hilo lilitokea
juzi saa tisa usiku katika Kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Usiulize
Kata ya Mwamalole.
Alisema
katika tukio hilo, wapenzi wawili Jumanne Gunda (39), mkazi wa Kijiji
cha Kinyambuli wilayani Mkalamo, akiwa amelala na mchumba wake, Mariamu
Khamis (49) mkazi wa Kijiji cha Ibaga Wilaya ya Mkalamo mkoani Singida,
kulitokea kutoelewana kati yao na kusababisha wagombane.
Katika ugomvi
huo, ambao chanzo chake ni wivu wa kimapenzi, Mariamu anatuhumiwa
kuzivuta korodani za mpenzi wake na kusababisha mishipa muhimu kukatika
na kusababisha kifo cha Jumanne papo hapo.
Kufuatia kifo
hicho, Mariamu aliburuza mwili wa mpenzi wake mpaka chooni kwa lengo la
kuutumbukiza katika shimo la choo. Hata hivyo kutokana na udogo wa tundu
la choo, alishindwa kutumbukiza mwili huo chooni na hivyo kuamua
kuutelekeza humo.
Asubuhi
kulipopambazuka, majirani wa nyumba waligundua mwili wa marehemu ukiwa
umetelekezwa chooni na kutoa taarifa Kituo cha Polisi, ambao walifika
katika eneo la tukio na kumtafuta mtuhumiwa, Mariamu.
Baada ya
Mariamu kukamatwa, anatuhumiwa kukiri kumuua mpenzi wake katika ugomvi
kati yao, uliotokea usiku walipokuwa wamelala wote wawili. Anatuhumiwa
kukiri kumvuta korodani zake na kusababisha kifo chake.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII