UKISTAAJABU YA MUSA BASI NDO HAYA : MTOTO AISHI NA CHATU, AMEKUWA KAMA NDUGU YAKE. SOMA ZAIDI HAPA




Ukistaajabu ya Musa basi ya Filauni ndo utakufa kabisaa!! Mtoto wa miaka 13 aitwaye Bingze kutoka China Jimbo la Guangdong amekuwa akiishi na chatu toka akiwa mtoto. Baba wa mtoto huyo anasema chatu huyo amekuwa sehemu ya familia na wameishi naye kwa miaka 19. Chatu huyo amekuwa akiachwa na mtoto toka akiwa mdogo na ndio amekuwa kama mlezi wake kwa sababu wazazi wa mtoto huyo wako bize sana katika kazi zao wanazofanya huko katika mji wa Binghze

Baba mtu alivyohojiwa alisema anafuraha sana kwa uwepo wa chatu huyo katika familia yake maana amekuwa akimfariji mwanaye na wamekuwa wakicheza wote mara kwa mara, na hasahasa akichoka mtoto huyohumgeuza chatu huyo kama mto wa kulalia......DUUUH

HAYA NDIO MAAJABU YA DUNIA, WE UNAWEZA KUMWACHA MWANAO HATA NA NYOKA MDOGO TU?????

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

2 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs