WASANII 10 WA KIKE WA BONGOMOVIE WALIOFANYA VIZURI ZAIDI MWAKA HUU NDIO HAWA

Hii ni orodha ya waigizaji wa kike nchini waliofanya vizuri mwaka 2013. Orodha imeandaliwa   kwa msaada mitandao inayoandika habari za filamu nchini, wadau mbalimbali wa filamu pamoja na makampuni ya kusambaza filamu nchini.

SHAMSA FORD.
  Shamsa_ford2
Shamsa amefanya poa sana mwaka huu katika filamu nyingi. Katika filamu ya ‘Bado Natafuta’ ameonyesha uwezo wake na kuwavutia wengi.Filamu nyingine alizofanya kwa mwaka huu ni Shikamoo Mzee,Zawadi Yangu pamoja na Impossible.


IRENE PAUL. 


  Irene-Bahati-Paul-cut
Irene ni mmoja ya msanii wa filamu ambao ameoneka kukubalika sokoni. Mwaka 2013 ametamba katika filamu ya Majuto na Best Losers,Fiona,Chinga Codineta, Love & Power, Kalunde zingine.


RIYAMA ALLY.

  RIYAMA-ALLI-CUT
Riyama mwaka huu ametamba na filamu kama Nimekuchoka, King’amuzi, Nipe Ripoti, My Enemy, Magata, Kovu La Siri ambazo zimemfanya mwaka huu aonekane ni mmoja wa waigizaji waliofanya vizuri 2013.


JACKY WOLPER  wolper-1
Jacky ni msanii wa filamu ambaye kwa mwaka huu amefanya filamu kama After Death,Crazy Desire,Mbegu, Pain for Pain P.F.P na nyingine nyingi. 


JOHARI 
clip_image001_thumb[2]
Johari ni mmoja wa wasanii wa filamu wa kike waliofanya kazi nyingi na marehemu Steven Kanumba lakini mpaka leo bado uwezo wake ni mzuri.Mwaka huu Johari amefanya filamu kama Mr. Masumbuko, Bad Luck, Rudi Kaburini, Vagabond na zingine.


YVONNE CHERRYL(MONALISA)  

  Yvonne-Cherryl-Monalisa-480x511
Mwanadada huyu bado anaendelea kufanya vizuri kadri siku zinapozidi kwenda.Mwaka huu amefanya filamu kama Daladala, Mwisho Wa Siku na pia kung’ara kwenye tamthilia ya ‘Siri Ya Mtungi’ iliyotajwa kuwania tuzo saba za Africa Magic.


ELIZABETH MICHAEL(LULU)  Lulu
Pamoja na kutoa filamu chache mwaka huu, Lulu ni msanii wa filamu maarufu zaidi baada ya Wema Sepetu. Mwaka huu ametamba na filamu yake ya Foolish Age ambayo ilifanya vizuri sokoni.

CATHY RUPIA 

  CATHY RUPIA
Cathy ni mmoja kati ya waigizaji wazuri. Mwaka huu amefanya filamu kama Melvin, Bad Luck, Pain Killer, Zulfa,Without Daddy, Nesi Selena na zingine.


 

AUNT EZEKIEL

  AUNT EZEKIEL
Mwaka huu ametamba na filamu kama Scola, Prison Revenge,Last Step,Pumba,Radio Presenter pamoja na nyingine nyingi.

WASTARA JUMA   wastara
Ni mwigizaji wa siku nyingi sana,kwa mwaka huu ameonyesha kufanya vizuri katika filamu kama Kivuli ana Shaymaa ambazo zipo sokoni kwa sasa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs