KIOJA: MCHUNGAJI AFA MAJI BAADA YA KUJARIBU KUTEMBEA JUU YA MAJI KAMA YESU, SOMA HAPA

NIGERIA. Ilikuwa sikitisho kubwa kwa waumini baada ya mchungaji wao kusombwa na maji baada ya kujaribu kutembea juu ya maji kama vile masihi Yesu alivyofanya wakati wake alipokuwa duniani.

Pastor Frank Kabele mwenye umri wa miaka 35, aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani. Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake.

Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya pastor huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs