KWA MARA YA KWANZA : MPENZI WA JACK CLIFF JUX AFUNGUKA KUHUSU MPENZI WAKE KUKAMATWA NA MADAWA CHINA

Muimbaji wa kundi la Wakacha, Jux amefunguka kwa mara ya kwanza tangu mpenzi wake Jackie Cliff akamatwe na madawa ya kulevya aina ya heroin huko Macau, China, December mwaka jana. 

Jackie alikamatwa na madawa hayo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 220 akitokea Thailand.
Jux ambaye hajawahi kuuweka wazi uhusiano wake na Jackie jana alipost picha akiwa amekaa nje ya gari lililo mlango wazi huku akiwa amejiinamia na kuandika: Kila kitu kinatokea kwa sababu kwenye maisha.”
Hadi sasa hatma ya Jackie nchini China haijulikani na bado anashikiliwa napolisi. Kuna uwezekano mkubwa akafungwa jela huko huko.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs