TAZAMA PICHA ZA MAZISHI YA MPIGA DRUMS WA TWANGA, MCD....PICHA ZIPO HAPA
Marehemu Masoud Mohamed MC D enzi za uhai wake.
Marehemu
Masoud Mohamed maarufu kama MC D mpiga tumba wa Bendi ya Twanga Pepeta
amezikwa leo Saa Saba katika Makaburi ya Njoro yaliyopo Moshi Mkoani
Kilimanjaro. Katika Mazishi ya Mwanamuziki huyo wadau mbalimbali wa
muziki wa Dansi waliungana pamoja kumsindikiza MC D katika safari yake
ya Mwisho. Marehemu MC D alifariki Siku ya juma tatu saa nne usiku
katika Hospitali ya KCMC dakika chache baada ya kufikishwa hapo kwa
matibabu. Hata hivyo wanamuziki wa bendi mbalimbali walikua wakimlilia
huku wakikiri ya kuwa hakuna mpiga Tumba mahiri kama yeye na Kifo chake
kimeacha pengo kubwa katika muziki wa dansi.
Ndugu na Jamaa wakiwa wanasubiri mwili wa MC D uandaliwe na kuwekwa katika Jeneza Tayari kwa Maziko.
Mpiga
Drums wa Twanga Pepeta mwenye miwani nyeusi anayefahamika kwa Jina la
MKIBOSHOO akiwa nje ya Nyumba ya kina MC D tayari kwa kumsindikiza
Mwanamuziki mwenzake.
Baadhi
ya wanamuziki na wapenzi wa muziki wa Dansi wakiwa wamekaa kwa majonzi
eneo la nje la Msikiti wa Rahma uliopo Moshi ambapo Mwili wa Marehemu
ulikua ukisaliwa kwa mara ya mwisho.
Wanamuziki na mdau wa Muziki wa Dansi Bahati aliyeweka mkono mfukoni wakijadili jambo nje ya msikiti wa Rahma.
Safari ya kuupeleka mwili wa MC D makaburini
Umati wa watu ukiusindikiza Mwili wa Marehemu MC D kuelekea Makaburini
Safari ya kuelekea Makaburi ya Njoro mahali atakapolazwa MC D
Hii ndiyo nyumba ya Mwisho atakapolazwa MC D
Mwili wa Marehemu MC D ukitolewa katika Jeneza tayari kwa kuzikwa.
Mwili wa MC D ukihifadhiwa kaburini kwa Taratibu za Kiislam
Mdau wa Muziki wa Dansi Tanzania Ndugu Patrick Kisaka maarufu kama Dozee akishuhudia Mwili wa MC D ukihifadhiwa Kaburini.
Wanamuziki wa Twanga Pepeta wakiwa kwa ukaribu katika shughuli ya kumuhifadhi mwanamuziki mwenzao marehemu MC D.
Umati wa watu ukiwa katika makaburi ya njoro katika safari ya mwisho ya MC D
Shughuli ya kurudisha udongo Kwenye kaburi ikiendelea.
Hii ndiyo nyumba ya Milele ya Mwanamuziki Nguli na Mpiga Tumba Maarufu Tanzania MC D
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII