Mkono asalimu amri baada ya kukatwa wazazi CCM

Mzee Mkono akiteta Jambo na JK
Mmoja ya watu walijitokeza kugombea uenyekiti kupitia jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi-Taifa, Nimrod Mkono, amesema anaunga mkono kwa asilimia mia moja maamzi yote ya vikao vya uteuzi wa wagombea.

Alisema kuteuliwa yeye hakuna maana kuwa kuna jambo limekosewa bali ni taratibu za chama na kwamba kwa asilimia mia moja anaunga mkono uamuzi huo ambao umefanywa katika vikao mbalimbali vikiwemo vile vilivyokuwa chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete jana.

“Mimi ni Mwana-CCM damu. Ninaunga mkono uamuzi wa chama changu tena kwa asimia mia moja. Walioteuliwa ni WanaCCM wenzangu. Ninatoa ahadi ya kuwapa ushirikiano wa kutosha hadi tutakapo pata mmoja wetu kuwa kiongozi wa Jumuiya yetu,” alisema Mkono.

Kuhusu kauli yake kuwa endapo hatapitishwa jina lake “hapatatosha” ndani ya CCM, a lisema kauli ile, “Nilisema sikubaliani na yale yaliandikwa kwenye magazeti kwani wakati mchujo unafanyika sikuwepo hivyo huwezi kusema nilikuwa wa mwisho wakati hata sikuwepo, ndiyo maana nilisema sikubali kama kweli imekuwa hivyo kwa kuwa sikuwepo ila nilijua uamuzi ninaoungoja ni wa vikao vingine na uamuzi umefanyika kwa haki na nimeridhika bila kinyongo, hivyo ni wajibu wangu kukisaidia chama changu,” alisema Mkono.

Aidha, kuhusu kauli ya mwenyekiti wake wa Taifa kuwa watakaoshindwa kupitishwa watakihama chama hicho na kuwataka waende mapema, alisema hiyo ni kauli ya kiongozi wake ambayo yeye hajawahi kuitoa popote wala kutoa vitisho vya namna hiyo kwa chama chake

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs