CHADEMA YAPINGA MABALIKO YA IGP MWEMA, YAHOJI KUHUSU KAMANDA KAMUHANDA...
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepinga uteuzi uliofanywa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Saidi Mwema kwa madai kwamba haukidhi ufa unaoliandama jeshi hilo wa kashfa za mauaji na utekaji.
Tamko la chama hicho limekuja baada ya IGP Mwema
kufanya mabadiliko kwenye safu ya makamanda na maofisa mbalimbali bila
kumgusa wa Iringa, Michael Kamuhanda ambaye amekuwa akiwekewa shinikizo
la kuwajibishwa.
“IGP Mwema anaendelea kupanga na kupangua safu
yake bila kuzingatia ukweli kuwa Jeshi hilo analoliongoza, liko katikati
ya tuhuma za mauaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu," alisema
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare.
Alidai: Uteuzi wowote unaofanyika bila kuzingatia
ukweli huo, hauwezi kuondoa doa kubwa linaloandama jeshi hilo mbele ya
macho ya Watanzania."
Lwakatare ambaye alitoa maelezo hayo kupitia
taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema Chadema ingetarajia
mabadiliko ya kulisuka upya jeshi hilo kwa kubadili makamanda na
maofiosa wengine.
“Uteuzi huu wa IGP Mwema umezidi kudhihirisha
namna Serikali ya CCM inavyozidi kupalilia na kukomaza mizizi ya tabia
ya kulindana, si katika ufisadi wa mali za umma tu, bali hata katika
roho za watu, hasa raia wa kawaida," alisema Lwakatare.
Alisema kuwa Kamati Kuu ya Chadema pamoja na
Barua ya Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe kwenda kwa Rais, kumtaka
Rais Kikwete ilimtaka awawajibishe viongozi wa juu wa Wizara ya mambo ya
ndani kutokana na mauaji yaliyotokea Arusha, Morogoro na Iringa.
Alitaja baadhi ya matukio hayo kuwa ni Januari 5, mwaka huu ambapo watu watatu waliuwawa mkoani Arusha na mto mmoja aliyeuawa Agosti 27 mkoani Morogoro na Mwanindishi wa Habari mkoani Iringa Septemba, 2
Alitaja baadhi ya matukio hayo kuwa ni Januari 5, mwaka huu ambapo watu watatu waliuwawa mkoani Arusha na mto mmoja aliyeuawa Agosti 27 mkoani Morogoro na Mwanindishi wa Habari mkoani Iringa Septemba, 2
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII