HUU NDIO UTAJIRI WA MWANAMUZIKI CELIN DION.....ANAMILIKI NDEGE, NA MIRADI MINGI..

MONTREAL, Canada 
CELINE Dion ni mwanamuziki wa Canada, ambaye ana jina kubwa katika medani ya muziki akiamianika kuwa ndiye anayeshikilia rekodi ya kuuza kazi nyingi zaidi za muziki. 

Dion ambaye alianza shughuli za muziki akiwa na umri wa miaka mitano, ana utajiri wa kiasi cha Dola 600 milioni (Sh 50 bilioni za Kenya). 

Mkali huyo anasifika kwa sauti nzuri huku akiwa mahiri wa kuimba muziki wa taratibu, R&B na wakati mwingine classical. 

Aliibuka zaidi mwaka 1990 wakati alipoachia albamu ya Unison na kumfanya ajizolee sifa katika nchi za Marekani, Canada na nchi za Jumuiya ya Madola. 

 Jina la Dion lilijulikana zaidi katika miaka ya 1980 baada ya kushinda mashindano ya kuimba ya Yamaha World Popular Song Festival mwaka 1982 na yale ya Eurovision baada ya kuiwakilisha Uswisi mwaka 1980. 
Hata hivyo, wimbo wa 'My Heart Will Go On' uliotumika katika filamu ya Titanic ndio uliompa chati zaidi katika medani ya muziki. 

Dion anashikilia rekodi ya kuwa mwanamke pekee, ambaye aliuza zaidi ya nakala milioni 200 duniani kote. 

Mwanamuziki huyo ametengeneza utajiri wake kutokana na biashara ya migawaha. Ana migawaha kadhaa nchini Canada iliyo chini ya kampuni yake ya Nickel Restaurants. 
 
Dion anamiliki jumba kubwa katika mji wa Montreal, Quebec ikiwa na thamani ya Dola 29 milioni (Sh 2.5 bilioni za Kenya)
Nyumba huyo ina vyumba sita vya kulala, sehemu ya chakula, jiko, maktaba, gym na sehemu ya kuogelea. 

Pia jumba jingine nchini Ufaransa katika eneo la Montmorency kwenye jiji la Paris likiwa na thamani ya Dola 47 milioni (Sh bilioni nne za Kenya). 
Anamiliki nyumba nyingine katika eneo la Notre-Dame De La Merci lililoko katika mji wa Quebec, Canada. 

Dion anamiliki pia klabu ya Le Mirage, ambayo ina eneo kubwa la kucheza mchezo wa gofu huko Quebec. Aliwekeza kiasi cha Dola 15 milioni (Sh 1.4 bilioni za Kenya) katika klabu hiyo. 
 
Dion anamiliki magari kadhaa lakini mojawapo aina ya Royal Royce Corniche, ambalo limebuniwa na Bill Allen. 

Pia anamiliki ndege aina ya Bombardier, ambayo ina vikolombwezo mbalimbali. Ndege kama hiyo wanayo matajiri Bill Gates na Steven Spielberg. 


The aircraft, operated by Vesey Air on behalf of owner Celine Dion

 

Dion na Rene Angelil walikutana mwaka 1980 wakati Dion akiwa na umri wa miaka 12. Walioana Aprili 17, 1994, katika kanisa la Notre-Dame Basilica mjini Montreal, Quebec.
 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs