BARNABA NA LINAH WA THT WAITOLEA NJE SHOW YA LADY JAY DEE
Linah na Barnaba wameiambia Bongo5 
kuwa hawatakuwepo kwenye show ya miaka 13 ya muziki ya Lady Jaydee 
itakayofanyika May 31, kwa kile walichodai ni kutoafikiana kwenye 
malipo.

Wamesema licha ya kuendelea kuwepo kwa majina yao kwenye poster ya show hiyo, hawatotumbuiza siku hiyo.
“Dada yetu alituita, akatuambia 
kwamba ana kazi yake ya kutumiza miaka 13 kwahiyo akawa anasema 
anahitaji wasanii ambao watamsupport kwaajili ya kufanya show,” amesema 
Linah. “Sisi tulifuata protocol zote kwasababu kama wasanii tuna 
viongozi, tukafuata protocol zote kuweza kukubaliana naye mpaka 
tukafikia hatua kwenye masuala ya biashara, yaani malipo. Kwenye upande 
huo kidogo tukawa tumepishana, kwenye upande wa masuala ya maslahi. 
Lakini sasa tunashangaa yeye kuanza kuweka posters.”
Kwa upande wake Barnaba amesema 
hawajashindwana na Lady Jaydee lakini wao kama wasanii wana menejementi 
na matakwa ya ofisi zao na hivyo muafaka ulishindwa kufikiwa na pia 
walikuwa na booking zingine.
Hata hivyo Barnaba amesema hakuna 
ugomvi wowote baina yao na Lady Jaydee. “Tuko safi tu na dada, mbona 
tuliafikiana vizuri tu na tuko kwenye maongezi mazuri tu, tulishaongea 
na hili suala liko vizuri,” amesema Barnaba.
 
 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII