MAUAJI HAYA MPAKA LINI?? WATOTO WA DIWANI WA CCM HUKO MBEYA WAUAWA KWA KUNYONGWA..SOMA ZAIDI
Diwani
wa kata ya Nkangamo Weston Simwelu akifarijiwa na Diwani mwenzake wa
Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka mara baada ya Bw. Simwelu kufiwa na
watoto wake wawili kwa kuchinjwa na kunyongwa
Katibu Uchumi
na Fedha wa Kata ya Tunduma akimfariji Diwani wa Nkangamo Weston Simwelu
ambaye watoto wake waliuawa kinyama kwa kuchinjwa na kunyongwa mjini
Tunduma.
Mke
wa Diwani wa kata ya Nkangamo Tumaini Yohana akifarijiwa na ndugu na
jamaa mara baada ya kutokea kwa mauaji ya kinyama nyumbani kwake ambapo
mwanaye aliuawa kwa kuchinjwa na mfanyakazi wake wa ndani aliuawa kwa
kunyongwa.
Jeneza lenye
mwili wa msichana wa kazi wa Bw. Simwelu, Sista Nyirenge likiwa tayari
kwa kusafirishwa kwa ajili ya mazishi katika kijiji cha Isansa wilayani
Mbozi
Diwani wa kata
ya Tunduma Frank Mwakajoka (kulia) na kiongozi wa mtaa huo Stanslaus
Malekela wakiwa wanamuongoza Diwani wa Nkangamo Weston Simwelu ambaye
alipata pigo la kuuawa kwa watoto wawili.
Baadhi ya majirani wa mtaa wa Tazara ambao walifika eneo la tukio kushuhudia mauaji hayo.
Kaka wa marehemu Sista Nyirenge, Mashaka Nyirenge akiwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti kituo cha Afya Tunduma.
Msafara
kuelekea kijiji cha Isansa kwa ajili ya mazishi yalyotokana na vifo
vilivyotokana na mauaji ya kinyama yaliyofanyika mjini Tunduma mkoani
Mbeya.
WATOTO wawili wa Diwani wa Kata ya Nkangamo wilayani Momba mkoani Mbeya
Weston Simwelu(55) wameuawa kikatili na watu wasiofahamika kwa kuchinjwa
na kunyongwa baada ya kuvamiwa majira ya saa 8:00 mchana Disemba 19
nyumbani kwao eneo la Tazara katika mji mdogo wa Tunduma uliopo mpakani
mwa Tanzania na Zambia.
Mauaji hayo ya kutisha yameteka hisia za wakazi wa eneo hilo kwa madai
kuwa huenda yanahusishwa na imani za nguvu za giza huku baadhi wakidai
kuwa yametokana na mgogoro wa kifamilia.
Taarifa za awali katika eneo la tukio zimedai kuwa Diwani huyo alikuwa
akiishi na mke mdogo aliyefahamika kwa jina la Tumaini Yohana(29) ambaye
ni mfanyakazi katika halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma ambaye wakati
wa tukio hilo alikuwa kazini.
Imeelezwa kuwa chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa ni kitendo cha Diwani
huyo kuwa mbali na mke mkubwa kwa muda mrefu huku ikidaiwa kuwa mke
mkubwa amenyimwa mali za mumewe yakiwemo mashamba na nyumba.
Jeshi la Polisi kupitia Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Barakael
Masaki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja marehemu kuwa ni
Kalibu Simwelu(6) ambaye aliuawa kwa kuchinjwa shingoni kwa kutumia
kisu na watu wasiofahamika ambapo mtu mwingine aliyeuawa ni mfanyakazi
wa ndani aliyetambulika kwa jina la Sista Nyilenda(17).
Kamanda Masaki alisema kuwa Mfanyakazi wa ndani aliuawa kwa kunyongwa
kwa kutumia waya wa televisheni iliyokuwepo sebuleni ambapo wauaji
wanadaiwa kuwavamia na kuwaua kinyama ambapo miili ya marehemu ilikutwa
sebuleni.
Alisema kuwa wakati wa tukio hilo baba wa watoto hao Bw. Simwelu alikuwa
shambani katika kijiji cha Kipaka wilayani humo ilhali mama wa mtoto
Tumaini alikuwa kazini kwake ofisi ya Halmashauri ya Mji mdogo wa
Tunduma.
Aidha katika tukio hilo Kamanda Masaki alisema kuwa mbali na kufanya
mauaji hayo, wauaji waliiba mabegi makubwa mawili yenye nguo mbalimbali
ambayo yalikuwa katika chumba wanacholala watoto.
Kamanda Masaki alisema kuwa kufuatia mauaji hayo watuhumiwa watano
wametiwa mbaroni ambao ni Gabriel Simwelu(19)Enock Simwelu(23) na Alex
Simwelu(16) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya
Sekondari Mpakani ambao wote ni watoto wa mke mkubwa wa Bw. Simwelu.
Wengine waliokamatwa ni pamoja na Mussa Ngoba(19) mkazi wa mtaa wa Mwaka
na Patrick Msigwa(18) mkazi wa mtaa wa Majengo na kwamba miili ya
marehemu imehifadhiwa katika kituo cha Afya Tunduma.
Picha na habari kwa hisani ya Mkwinda Blog
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII