‘AMINI’ AJIBU MAPIGO YA ‘LINAH’…..”NGOMA YANGU MPYA YA ‘KIMBELEMBELE’ INAZUNGUMZIA NILIVYOUMIZWA KWA KUMPENDA STAA” – AMINI…!!

BongoNewz
MSANII anayefanya vizuri kwenye muziki wa bongo fleva kutokana na nyimbo zake za mapenzi Amini alizungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano na mtandao wa DarTalk, alisema kuwa ngoma mpya ya ‘Kimbelembele’ , inazungumzia namna alivyoumizwa na mahusiano hasa yale ya kutoka na mwenye jina na kuonekana yeye ni kimbelembele.

Ngoma hiyo kinazungumzia namna alivyoanza mapenzi pindi alipoingia kwenye tasnia ya muziki, ambapo baadhi ya mistari inasema kuwa “Wiki ya kwanza nilimpenda mwenye jina na nilipomuita jina lake alikataa na wiki nyingine nikampenda mwenye jina ’shida’ na kulipa luku ikawa shida” ni moja ya ujume mzito unaopatikana ndani ya ngoma hiyo.

Kutokana na maneno hayo wimbo huo unaonesha wazi kuwa wiki ya kwanza alikuwa na mahusiano na msanii mwenzake ‘Linah’ na walikuja kuachana baada ya mwanadada huyo kujiona ni staa ambapo hali ilikuja kujitokeza kwa mara ya pili baada ya kuwa katika mahusiano na mtoto ambaye kwao kulikuwa na matizo makubwa naye hakudumu naye.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs