Mamlaka za Tanzania zatahadharisha kuhusu dawa za kughushi za UKIMWI
BongoNewz
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ilitahadharisha siku ya Alhamisi (tarehe 20 Septemba) kwamba dawa za kughushi za kupunguza makali ya VVU zipo katika mzunguko na kwamba watu hadi 495,000 wanaweza kuwa hatarini, gazeti la The Citizen la Tanzania liliripoti.
TFDA ilitangaza kwamba dawa zenye jina la TT-VIR 30 zimebainishwa kama ni mchanganjiko wa dawa nyingine, na imeziagiza hospitali nchi nzima kuacha kuzitoa, na kurejesha zile zilizobaki katika mamlaka zinazohusika. Dawa za TT-VIR 30 zilisambazwa nchini kote kabla hazijajulikana kuwa ni za kughushi, na zimepatikana katika hospitali za Dar es Salaam, Tanga na Mara.
Kati ya Watanzania 900,000 walioandikishwa kuwa ni wagonjwa wa UKIMWI, asilimia 55 walipewa maelekezo ya kutumia dawa za TT-VIR 30, alisema Fatuma Mrisho, Mwenyekiti wa Tume ya Kupambana na UKIMWI Tanzania.
Watengenezaji wanaohusika na kughushi huko bado hawajabainishwa, ingawa uchunguzi unaonyesha kwamba zaidi ya bechi moja ya dawa hizo haifai kwa matumizi ya binadamu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII