CCM wakiri Kuelemewa na CHADEMA...'Hali tete'
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), sasa kimekiri kuelemewa na wimbi la kukimbiwa na wanachama wake hususan vijana wanaojiunga na vyama vya upinzani baada ya kuona matarajio yao hayapatikani ndani ya chama hicho.
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Mbeya Dk. Steven Mwakajumilo pamoja na kukiri hali hiyo, alionya kuwa ikiwa chama hicho kinataka kuendelea kuungwa mkono, lazima kichukue hatua za makusudi za kukabiliana na hali ngumu ya maisha ya Watanzania.
Dk. Mwwakajumilo alisema hayo juzi wakati akiendesha harambee ya mfuko wa vijana wa chama hicho, katika kata ya Ihyela, jijini Mbeya.
Alisema kuwa vijana wengi nchini kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya kiuchumi, hivyo kuwakatisha tamaa.
“Vijana wengi wamekimbilia upinzani pengine kwa kuona matarajio yao hayapatikani ndani chama, tunazo sera nzuri sana ndani ya CCM za kumkwamua kijana kiuchumi, lakini inawezekana wimbo tunaoimba ni tofauti na ule tunaoucheza,” alisema Dk. Mwakajumilo.
Dk. Mwakajumilo ambaye pia ni mchumi na mtumishi wa Benki Kuu ya Tanzania alitoa wito kwa kila tawi la CCM mahali lilipo kujizatiti kwa kuanzisha vikundi vya vijana vya ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wa kiuchumi sambamba na kulipatia uwezo tawi husika kufanya shughuli za maendeleo ya chama.
“Kila tawi la CCM mahali lilipo lijizatiti kuanzisha vikundi vya ujasiriamali, ndipo litakuwa na uwezo hata wa kujenga nyumba na ofisi za chama,” alisema Dk. Mwakajumilo.
Dk. Mwakajumilo aliahidi kufanya operesheni ya kuanzisha vikundi hivyo vya ujasiriamali katika kila tawi la CCM ndani ya kata ya Ihyela jijini Mbeya ili kuonyesha mfano wa uanzishwaji wa vikundi hivyo. Chanzo GAZETI (Tanzania daima). TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Mbeya Dk. Steven Mwakajumilo pamoja na kukiri hali hiyo, alionya kuwa ikiwa chama hicho kinataka kuendelea kuungwa mkono, lazima kichukue hatua za makusudi za kukabiliana na hali ngumu ya maisha ya Watanzania.
Dk. Mwwakajumilo alisema hayo juzi wakati akiendesha harambee ya mfuko wa vijana wa chama hicho, katika kata ya Ihyela, jijini Mbeya.
Alisema kuwa vijana wengi nchini kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya kiuchumi, hivyo kuwakatisha tamaa.
“Vijana wengi wamekimbilia upinzani pengine kwa kuona matarajio yao hayapatikani ndani chama, tunazo sera nzuri sana ndani ya CCM za kumkwamua kijana kiuchumi, lakini inawezekana wimbo tunaoimba ni tofauti na ule tunaoucheza,” alisema Dk. Mwakajumilo.
Dk. Mwakajumilo ambaye pia ni mchumi na mtumishi wa Benki Kuu ya Tanzania alitoa wito kwa kila tawi la CCM mahali lilipo kujizatiti kwa kuanzisha vikundi vya vijana vya ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wa kiuchumi sambamba na kulipatia uwezo tawi husika kufanya shughuli za maendeleo ya chama.
“Kila tawi la CCM mahali lilipo lijizatiti kuanzisha vikundi vya ujasiriamali, ndipo litakuwa na uwezo hata wa kujenga nyumba na ofisi za chama,” alisema Dk. Mwakajumilo.
Dk. Mwakajumilo aliahidi kufanya operesheni ya kuanzisha vikundi hivyo vya ujasiriamali katika kila tawi la CCM ndani ya kata ya Ihyela jijini Mbeya ili kuonyesha mfano wa uanzishwaji wa vikundi hivyo. Chanzo GAZETI (Tanzania daima).
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII