HAYA NDO MAISHA YA DJ FETTY
BongoNewz
SAFARI ni safari hata kama ni kwa Baiskel,Bodaboda,Gari au kwa miguu hiyo bado itaitwa ni safari tu.siku zote mwanadamu anpoanza safari ya kuitafuta ndoto yake itamlazimu ajitume kwa bidii ili aweze kufika.
Nikitaja majina ya Watangazaji na Madj’s ambao ni kipenzi cha mashabiki wengi wa muziki walioko kwenye chat kwa hapa nchini ni lazima utakutana na jina ‘Fetty’ hautalikosa katika ukurasa wowote wa burudani.Binti huyu ni shombeshombe wa kisomali aliyezaliwa Mkoani Shinyanga miaka fulani ya themanini japo si mksukuma.Baadaye akaingia jiji la Dar es Salaam ambapo alipata elimu yake yote ya sekondari.
‘Fetty’ anasema mwaka 2003 alivutia sana Babla Hassan wakati huo akitangaza kipindi cha ‘Hang out’ saa sita mpaka saa nane mchana kituo hicho cha Clouds Fm.
“Kiukweli alikuwa alinishawishi sana Safari ya kutimiza ndoto zangu za utangazaji, sikuwa nimesomea kazi hii lakini niliamini kuwa nitaweza mwaka wa 2004 nilienda ofisi za Clouds,niliomba kutangaza lakini haikuwa rahisi baadaye nilianza kuingia studio kumsikiliza Babla anavyotangaza”anasema Fet.
Kuanza kutangaza
Fetty anasema baada ya Babla kuacha kazi mwishoni mwa mwaka 2004 akitangaza kipindi hicho alikabidhiwa kukiendesha ndani ya masaa 3,bila kuongea hewani baadaye aliamua kuongea na Dj Nelly amfundishe kazi ya kuchezea sahani za muziki,alionekana kufanya vizuri na ilipofika mwaka 2006 mambo yakawa safi.“Nikaanza kusikika kidogo kidogo kwenye kipindi cha nyuki Dj’s ambapo kulikuwa na Jamaa sita na mtoto wa kike peke yangu,kipindi hicho kilikuwa siku ya Jumamosi ndani ya masaa 3 na nusu,ilipoanza julai 2006 tulianza kusikika mimi na ‘Muli B’
Anasema baada ya kufanya vizuri alipewa ofa ya kwenda Uingereza kusoma kozi fupi ya Utangazaji na alifanikiwa kurudi na wazo jipya la kipindi alichokiita ‘soso fresh’ kilicho maanisha kila kitu sawa ambacho kilifanya vizuri zaidi.
“Kipindi hicho nilikifanya kwa mwaka mmoja baadaye mabosi wakaona nafanya vizuri wakanipa majaribio ya miezi mitatu kipindi kikubwa cha ‘Top 20’ nikafanya vizuri,mashabiki walinikubali sana baadaye wakaona ‘bongo fleva’ inapwaya ambayo niliendelea nayo mpaka sasa.
Mafanikio yako
“Nia ya kuamua kufanya jambo fulani,Tamasha la Fiesta limenitoa sana ukiachana na kazi ya utangazaji japo ndio kazi iliyonijengea kwa mambo mengi,Tamasha la Fiesta ndio limefanya watu kunikubali zaidi,walikuwa wanamsikia fet kwenye Radio kwa hiyo wanaposikia tamasha wanatamani kumuona.nafasi ya Dj’s ni zaidi ya utangazaji kwangu.
Fetty anasema kupitia kazi ya utangazaji na Dj imemletea mafanikio ya kuwa na kampuni inayojulikana kwa jina la ‘fettylious’ inayohusika na matangazo na kutengezesha nembo za tishet.kwa hiyo anasema maisha yake ni mazuri kwa sababu anapata anachokita.
Ndoto zako
Tukiachana na tukio la kushangiliwa jumba la ‘Big Brother’ mwaka huu Fetty bado anatamani siku moja aweze kusikika kwenye Vituo vya Radio za kimataifa kama vile BBC na Aljazir,mbali na ndoto hizo anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyonayo kwa sasa kwani ametokea kuwa kipenzi cha watanzania wengi wanaopenda Muziki.
“Tukio la Dodoma miaka 10 ya fiesta nilishangaa watu walivyonipokea,walinitia moyo na kuamini kuwa ninapendwa yaani maelfu walitamani kunishika hata mkono lakini kilichosaidia ni askari.
Maisha yako na Jamii
“Yako poa sana ninaweza kujichanya na jamii yoyote hata tandale naishi,sipendi mtu anayefanikiwa na kusahau alikotokea kwa mfano unaenda Marekani miaka mitatu unarudi yes,no zinakuwa nyingi,unajifanya hujui tena kiswahili.
Fetty anasema yeye anaweza kuongea lugha ya kisukuma vizuri tu japo sio lugha yake pamoja kuishi mjini kwa mda mrefu.
Chakula anachopenda
“Hata kama nipo usingizini ukiniamsha usiku wa manane kama nina njaa nitakuomba Wali na Maharagwe ,ni chakula ambacho kwa kweli ninakipenda sana kelvin.
Una mchumba
“Da swali hilo kila mtu huwa anapenda kuniuliza lakini huwa sipendi kueleza chochote juu ya mahusiano yangu,wanaosema nina mtoto wa kigogo sio kweli maisha yangu yasingekuwa haya pengine ningekuwa namiliki Benzi au Vog’,sitaki kuweka wazi juu ya hilo.
Ila Fetty anapaza sauti mwanaume ambaye anaweza kuishi nae akisema ni yule ambaye ataweza kutoa ushirikiano katika kazi za ndani,anayemjali na kumthamini.
Ushauri kwa wanaopenda vya bure
Fetty anasema kila kitu ambacho kinapatikana kwa urahisi kina madhara hivyo anawashauri wanawake wanaojiuza miili yao kwa kigezo cha umasikini wafanye kazi,wajiunge kwenye makundi mbalimbali ya ujasiriamali.
“Uzuri usitudanganye,sidhani kama ni safi kama ukiwa mzuri harafu maskini,bora wanaume wakuone huwavutii lakini una pesa yako,inajenga heshima kitaani,
“Wanawake tusipende kulia lia sana,nadhani msaada ambao mwanamke anahitaji ni ukombozi wa kifikra.tusitumie kigezo cha jinsia kutengeneza usawa hata kama mwanamke hana uwezo eti nafasi kwa sababu ya kuweka usawa.
Changamoto ya ajira nchini
“Watu ni kweli wengi hawana kazi lakini isiwe kigezo cha kukaa na kubweteka matokeo yake tunaingia kwenye makundi yasiyofaa,kazi ya uandishi wa habari itapanuka sana mfumo wa digitali utakapoanza ila watanzania tuna tatizo la ubunifu,wengi tuna ‘kopi na kupesti’
Taifa liweze kup[iga hatua ni lazima watu wawe wabunifu katika nyanja za kiuchumi,
Serikali yetu
“Da huwa sipendi sana kuzungumzia serikali lakini tatizo lililopo ni kwa wabunge wetu,wengi hawana uwezo wa kupambanua hoja na tatizo ni elimu,mbunge darasa la saba lazima katiba ijayo iweke kiwango cha elimu ya wabunge, Wabunge mbumbumbu tuwapige chini,mbunge akiwa hivyo hawezi kutunga hata sheria zenye manufaa kwetu.
Tanzania ya kesho
“Natamani sana kuona serikali inafanikiwa kuondoa changamoto ya foleni, yaani msongamano wa magari imekuwa kero kubwa inakwamisha mambo mengi,ufisadi unaongezeka wanakula pesa zetu kila kukicha,natamani kupata kiongozi atakaye maliza kero hizi. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

“Natamani sana kuona serikali inafanikiwa kuondoa changamoto ya foleni, yaani msongamano wa magari imekuwa kero kubwa inakwamisha mambo mengi,ufisadi unaongezeka wanakula pesa zetu kila kukicha,natamani kupata kiongozi atakaye maliza kero hizi.
Du pouwa kweli
ReplyDeletevery very interested.my self i like the way she understands and having an ability of analysing problems and how to overcome.big up sana fetty,she also inspired me alot however am now taking electrical engineering at dit. i go by da name costantino mnyanga.
ReplyDeleteYes mamie luv u much,yo my roll model one day takua kaa wew..Mungu a2pe uzima2,keep t up baby
ReplyDeleteUmetisha fetty.
ReplyDeleteWanawake wote wangekua namawazo Kama yako taifa licngekuwa hapa lilipo....big up mamie subra ndo Cri yamafanikio...
ReplyDelete