JK asema, watu wanamiliki viwanda vya kutunga Uongo Tanzania!!!

BongoNewz
                                        TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,Alhamisi, Septemba 20, 2012, ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Daraja laKigamboni, Dar es Salaam kwa kuwaonya watu ambao amewaeleza kuwa wanavyoviwanda vya kutunga uongo kuacha tabia hiyo na kuelekeza nguvu kwenyemaendeleo.

Aidha ,Rais Kikwete amewahakikishia wakazi wote wa Kigamboni ambao wanaondolewa katikamaeneo yao kwa ajili ya kupisha ujenzi wa daraja hilo na ujenzi wa Mji Mpya waKigamboni kuwa watalipwa stahili na haki zao zote.

Daraja hilo la Kigamboni ambalo wazo la kujengwa kwake lilibuniwa kwa mara ya kwanzazaidi ya miaka 30, tokea mwaka 1978, wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere, linajengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 214.6 na litakuwatayari katika muda wa miezi 36 ijayo, ingawa muda huo unaweza kupungua na kubakiamiezi 30.

Daraja hilo litapunguza adha ya usafiri kati ya Kigamboni na Dar es Salaam ambao kwasasa unategemea vivuko, ama boti ndogo, mitumbwi ama wenye magari kulazimikakufanya mzungumo wa kilomita 52. Kwa uamuzi wa sasa, wavuka kwa miguu ambaowatakuwa na njia maalum kwenye daraja hilo pamoja na waendesha baiskeliwatavuka bure bila malipo yoyote.

Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali haiwezi kudhulumuwananchi wake na hivyo watu wote ambao wanastahili fidia kutokana na ujenzi wadaraja hilo na mji mpya wa Kigamboni watalipwa haki na stahiki zao.

Rais Kikwete pia amewaonya watu ambao wamelifanya suala la kutunga na kusema uongokama sehemu ya utamaduni wao. “Watu wana viwanda vya kuzalisha uongo.Wanashinda wanasambaza uongo kwenye mitandao, kila mahali. Wamepata hata kusemakuwa mimi nimemuuzia George Bush eneo la Kigamboni. Bush aje kufanya niniKigamboni?”

Rais pia amesema kuwa wapo watu ambao hawapendi maendeleo ya nchi. “Wanatamanikila siku tushindwe kuwaletea wananchi maendeleo.Lakini watakufa kwa kihorokwa sababu hatutashindwa. Kila tulilosema tutalifanya, litafanyika”.

Amesema kuwa thamani kubwa ya vyama vya siasa ni maendeleo ya wananchi. “Lakiniwapo wenzetu ambao wanaudhika wakiona maendeleo. Wanapenda hata daraja hililisijengwe. Leo hawatalala usingizi. Kazi ya vyama vya siasa ni kuweka maslahiyetu sote mbele.”

Imetolewa na:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dares Salaam.
20Septemba, 2012
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs