Madaktari watibuana; Baada ya wenzao kuomba radhi, wengine wasema hawahusiki
BongoNewz
Jana Mwakilishi wa Madaktari kwa Vitendo, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Frank Kagoro, alisema tamko la kuomba radhi lililotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari walioathirika na mgomo, Paul Swakala, haliwahusu madaktari wote. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dk. Kagoro, alisema tamko lililotolewa na Swakala linakihusu kikundi cha watu wachache ambao nia yao haijafahamika sawasawa. Katika mkutano huo uliowajumuisha viongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Kagoro alisema kwa sasa siyo wakati wa madaktari hao kuomba msamaha, kwa sababu suala lao lipo kisheria na kinachosubiriwa ni Baraza la Madaktari Tanzania (MCT) kuwaita kwa ajili ya kuwahoji.
“Lile tamko siyo tamko letu wote, lile ni tamko la kikundi cha watu wachache ambao hatujui wana lengo gani na nia gani, lakini mkituuliza sisi tutawaambia tunasubiri tuitwe na MCT ili kuhojiwa.
“Mahali suala letu lilipofikia, halina lugha ya msamaha, ninachofahamu ni kwamba, sisi suala letu tunalishughulikia kwa kushirikiana na Jumuiya, kwani tumefikia katika hatua ya kusubiri kuitwa na MCT.
“Katika hili tulikubaliana kwamba, jumuiya itabeba gharama za kutafuta wanasheria, kwa hiyo, wale madaktari waliotoa lile tamko hatujui wana nia gani,” alisema Dk. Kagoro.
Akizungumzia suala hilo, Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Nchini, Dk. Godbless Charles, alisema kipindi hiki ni kipindi chao kutumia hekima na busara, kwani ni kipindi kigumu kwao. Kutokana na hali hiyo, alisema kuna kila sababu yeye na madaktari wenzake kuepuka tabia ya kutumiwa na kikundi cha watu wachache wanaofanya hivyo kwa masilahi yao binafsi.
“Tunapenda ieleweke kwamba, mgomo wa madaktari si tukio, bali ni mchakato ambao utaendelea kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ndiyo maana tumeshuhudia migomo katika nyakati tofauti pamoja na kujitokeza kikundi au mtu kutumiwa kuomba msamaha kwa lengo la kudhalilisha taaluma na kurudisha nyuma jitihada za kuboresha hali ya afya nchini na maslahi ya watumishi kwa ujumla.
“Unajua, hata sisi tunawashangaa wale ambao wameomba msamaha, sasa waliomba msamaha kwa kosa gani?
“Nasema hivyo kwa sababu sisi madaktari tulio chini ya usimamizi wa madaktari bingwa (interns), hatuwezi kufanya kazi bila usimamizi wa madaktari bingwa ambao wako katika mgomo.
“Kuhusu suala hili la interns ikumbukwe kwamba, Julai 10, mwaka huu, Baraza la Madaktari (MCT) lilitoa taarifa kwa umma, kwamba, limesitisha leseni za muda kwa madaktari walio chini ya mafunzo kwa vitendo.
“Pia MCT waliahidi kutuita mmoja mmoja kwa ajili ya kutuhoji hadi taratibu zote zitakapokamilika, lakini cha kushangaza hadi sasa ni miezi miwili imepita hakuna kinachoendelea.
“Katika vikao mbalimbali ambavyo tumefanya na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na idara zake, tumekuwa tukisisitiza kuwa, suala hilo lipo kisheria na Interns wasubiri kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa, hivyo tunaitaka MCT iharakishe kuwaita ili kuharakisha upatikanaji wa haki.
“Sisi tumejiandaa vya kutosha na taratibu za kisheria na tutahakikisha tunaweka mawakili pale interns watakapoanza kuhojiwa, kwa kuwa sheria inayounda MCT inatoa nafasi hiyo.
“Lakini hata ukiangalia hoja za hao walioomba msamaha hazina uzito wowote, huwezi kusema ulilazimishwa kugoma wakati mgomo umekwenda kwa vipindi vitatu mfululizo na ulishiriki, hizi ni sababu ambazo zinatupa wasiwasi kwamba kikundi hiki kina sababu zake zilizojificha,” alisema Dk. Charles.
Naye Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Dk. Edwin Chitage, alisema huenda tamko lile la madaktari lina misukumo ya nje.
“Katika mazingira kama haya, kila mtu ana uwezo wake wa kupokea jambo, kuna ambao wanaweza kuhimili mikikimikiki na wengine hawawezi, kwa hiyo wale sisi hatusemi kwamba tunawakana. Tunasema hatukubaliani nao na naamini siyo makubaliano ya interns wote,” alisema Dk. Chitage. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

“Katika mazingira kama haya, kila mtu ana uwezo wake wa kupokea jambo, kuna ambao wanaweza kuhimili mikikimikiki na wengine hawawezi, kwa hiyo wale sisi hatusemi kwamba tunawakana. Tunasema hatukubaliani nao na naamini siyo makubaliano ya interns wote,” alisema Dk. Chitage.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII