Mkapa Alalamikia Kutopewa Heshima
BongoNewz
RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, ameibuka na kusema kuwa, hivi sasa baadhi ya viongozi wa Serikali na viongozi wa dini, wamekuwa hawawathamini na kuwajali viongozi wastaafu. Amesema hali hiyo imekuwa ikitafsiriwa na kuonekana kuwa, viongozi hao hawana jipya mbele ya jamii. Rais Mkapa alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipokuwa akihutubia katika ibada maalumu ya kumbukumbu ya miaka 40 ya uaskofu wa Askofu Mstaafu Mathias Isuja wa Jimbo Katoliki Dodoma.
Mkapa alisema, kuna dhana iliyojengeka, kuwa viongozi waliostaafu wanakuwa hawana jipya na hawathaminiwi tena kutokana na kustaafu kwao kwa mujibu wa sheria. “Hivi sasa imezuka tabia kwa baadhi ya viongozi wa nchi na makanisa kuona kuwa mtu akistaafu basi anakosa hekima.
“Mtu akistaafu anaonekana kuwa ni mufilisi tu asiye na kitu na nataka mfahamu kuwa, kustaafu siyo kuchoka na wala michango ya wastaafu siyo mibovu bali inatakiwa kuangaliwa,’’ alisema Rais mstaafu Mkapa. Aidha, alisema nchi imekuwa ikikumbwa na matatizo kutokana na ubishi na ujuaji wa wananchi hali inayosababisha nchi isipige hatua ipasavyo katika maendeleo.
“Siku hizi watu hawaambiliki na chimbuko kubwa la matatizo ni ujuaji mwingi, kila mtu anaamini kuwa anajua, na hili jambo ni la hatari.
“Wengine hawakuwapo wakati nchi hii inapata uhuru na hata wakati uhuru unapiganiwa, wao waliikuta nchi ikiwa huru.
“Lakini utakuta wanasimulia mambo mengi ambayo hata hawayajui na hayana msingi wowote,” alisema Mkapa.
Aliwataka pia viongozi kujenga tabia ya kujifunza bila kuchoka na kwamba viongozi lazima wawe mfano kwa kupenda kusoma. Akimzungumzia Askofu Isuja, Mkapa alisema Isuja alikuwa ni kiunganishi cha wananchi wa Dodoma pamoja na Tanzania, kwani alipenda kufanya kazi zake kwa uwazi na ukweli wakati wote. Mimi namfananisha Askofu Isuja na mtumishi mwema katika shamba la bwana,” alisema. Kwa upande wake, Askofu Isuja aliwashukuru maaskofu wote, mapadre, watawa, waumini wa Kanisa Katoliki wakiwamo wa Jimbo la Dodoma na Serikali kwa kipindi chote walichompa ushirikiano wakati akitumikia Jimbo la Dodoma.
Askofu Isuja pia alihimiza amani nchini na kuwataka Watanzania kuwa na upendo bila kujali ubaguzi wowote miongoni mwao. Mbali na viongozi hao, katika ibada hiyo alikuwapo pia Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kardinali Pengo ambaye ndiye aliyeongoza ibada. Walikuwapo pia viongozi mbalimbali wa Kanisa Katoliki nchini, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, ameibuka na kusema kuwa, hivi sasa baadhi ya viongozi wa Serikali na viongozi wa dini, wamekuwa hawawathamini na kuwajali viongozi wastaafu. Amesema hali hiyo imekuwa ikitafsiriwa na kuonekana kuwa, viongozi hao hawana jipya mbele ya jamii. Rais Mkapa alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipokuwa akihutubia katika ibada maalumu ya kumbukumbu ya miaka 40 ya uaskofu wa Askofu Mstaafu Mathias Isuja wa Jimbo Katoliki Dodoma.
Mkapa alisema, kuna dhana iliyojengeka, kuwa viongozi waliostaafu wanakuwa hawana jipya na hawathaminiwi tena kutokana na kustaafu kwao kwa mujibu wa sheria. “Hivi sasa imezuka tabia kwa baadhi ya viongozi wa nchi na makanisa kuona kuwa mtu akistaafu basi anakosa hekima.
“Mtu akistaafu anaonekana kuwa ni mufilisi tu asiye na kitu na nataka mfahamu kuwa, kustaafu siyo kuchoka na wala michango ya wastaafu siyo mibovu bali inatakiwa kuangaliwa,’’ alisema Rais mstaafu Mkapa. Aidha, alisema nchi imekuwa ikikumbwa na matatizo kutokana na ubishi na ujuaji wa wananchi hali inayosababisha nchi isipige hatua ipasavyo katika maendeleo.
“Siku hizi watu hawaambiliki na chimbuko kubwa la matatizo ni ujuaji mwingi, kila mtu anaamini kuwa anajua, na hili jambo ni la hatari.
“Wengine hawakuwapo wakati nchi hii inapata uhuru na hata wakati uhuru unapiganiwa, wao waliikuta nchi ikiwa huru.
“Lakini utakuta wanasimulia mambo mengi ambayo hata hawayajui na hayana msingi wowote,” alisema Mkapa.
Aliwataka pia viongozi kujenga tabia ya kujifunza bila kuchoka na kwamba viongozi lazima wawe mfano kwa kupenda kusoma. Akimzungumzia Askofu Isuja, Mkapa alisema Isuja alikuwa ni kiunganishi cha wananchi wa Dodoma pamoja na Tanzania, kwani alipenda kufanya kazi zake kwa uwazi na ukweli wakati wote. Mimi namfananisha Askofu Isuja na mtumishi mwema katika shamba la bwana,” alisema. Kwa upande wake, Askofu Isuja aliwashukuru maaskofu wote, mapadre, watawa, waumini wa Kanisa Katoliki wakiwamo wa Jimbo la Dodoma na Serikali kwa kipindi chote walichompa ushirikiano wakati akitumikia Jimbo la Dodoma.
Askofu Isuja pia alihimiza amani nchini na kuwataka Watanzania kuwa na upendo bila kujali ubaguzi wowote miongoni mwao. Mbali na viongozi hao, katika ibada hiyo alikuwapo pia Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kardinali Pengo ambaye ndiye aliyeongoza ibada. Walikuwapo pia viongozi mbalimbali wa Kanisa Katoliki nchini, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII