PINDA KUMLEGEZA WAZIRI MAGUFULI
Kuna dalili kwamba
Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, huenda akalegea kuwabomolea nyumba
wananchi waliojenga katika maeneo ya hifadhi za barabara katika baadhi
ya maeneo nchini, baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuahidi
kumshawishi alegeze kamba.
Waziri Magufuli mara kwa mara amekuwa akisisitiza kuwa watu wote waliojenga katika maeneo ya hifadhi ya barabara lazima wabomoe nyumba zao na kuondoka vinginevyo serikali itazibomoa bila kuwalipa fidia.
Wakati Magufuli akiendelea kushikilia msimamo huo, Pinda amewaahidi wakazi wa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza kwamba atazungumza na Waziri huyo ili asibomoe nyumba ambazo zimejengwa kwenye hifadhi ya barabara wilayani humo.
Akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi kwenye uwanja wa Getrude Mongella mjini Nansio, Pinda alisema licha ya ukweli kwamba nyumba nyingi zimejengwa ndani ya hifadhi, lakini ameona si busara kuzibomoa kupisha upanuzi wa barabara.
Alisema kwamba baada ya kutembelea wilaya hiyo katika ziara ya kikazi, amejionea mwenyewe jinsi barabara za mji wa Nansio zilivyo finyu kutokana na nyumba nyingi kujengwa kwenye hifadhi, hali ambayo alisema endapo Dk. Magufuli ataingia wilayani humu kutekeleza sheria ni wazi atabomoa nyumba nyingi.
“Hakuna ubishi kwamba mnahitaji barabara nzuri, lakini suala la barabara pia lina kero zake, akija Magufuli hapa atawaambia anataka mita zake 30 kila upande wa barabara, lakini kwa jinsi nilivyoona, nyumba nyingi zitabomolewa,” alisema.
Hata hivyo, alisema kwamba kutokana na uhaba wa ardhi, ameona ni busara azungumze na Dk. Waziri Magufuli aangalie uwezekano wa kupindisha sheria ili wakazi wa Wilaya ya Ukerewe waliojenga kwenye hifadhi ya barabara wasibomolewe nyumba zao.
“Ni kweli kwamba ipo sheria, lakini ni lazima sheria hiyo imsaidie mwananchi, kwa hiyo suala hili mniachie nitakwenda kuongea na Magufuli kusudi aangalie nini cha kufanya kunusuru nyumba zenu nzuri nzuri nilizoziona zisibomolewe,” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu Pinda alibainisha kuwa Wilaya ya Ukerewe yenye wakazi wapatao 260,000 na eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 6,400, ni asilimia 10 pekee ndiyo nchi kavu na sehemu iliyobaki ni maji.
Kwa kuzingatia hali hiyo, alisema haoni kwa nini wananchi wabomolewe nyumba kwa ajili ya kupanua barabara hasa ikizingatiwa kuwa wilaya hiyo ni kisiwa, hivyo hakuna mahitaji makubwa ya barabara kuu.
Wakati huo huo, Pinda amesema Wilaya ya Ukerewe inastahili kupata meli mpya na kubwa zaidi ambayo itachukua nafasi ya meli ya muda mrefu MV Clarias na MV Butiama ambayo hivi sasa ni mbovu.
Alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, kujenga hoja kuishawishi serikali ili ipeleke meli hiyo mapema iwezekanavyo.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII