Vikosi vya AU vyawadhibiti Al Shaabab Somalia
Vikosi vya Umoja wa Afrika na Somalia viliuteka mji wa Miido katika mapigano ya usiku ambayo yalianza jioni ya Ijumaa (tarehe 31 Agosti), na kuua wanamgambo 36 wa al-Shabaab, wenye mafungamano na al-Qaida, Misheni ya Umoja wa Afrika Somali (AMISOM) ilitangaza.
Mji wa Miido upo kilomita 16 kusini ya Afmadow, ambao karibuni ulikombolewa na majeshi ya AMISOM.
“Hii ilikuwa operesheni ya kishujaa na muhimu iliyofanywa na vikosi vya AMISOM katika Juba ya Chini,” alisema Kamanda wa AMISOM Luteni Jenerali Andrew Gutti. "Kuukomboa mji wa kimkakati wa Miido kutairuhusu jamii ya eneo hilo kujenga upya maisha yao wakiwa huru na ugaidi na udhalimu uliokuwa unafanywa na al-Shabaab. Ninaipongeza ushujaa na utendaji wa askari wote waliohusika na operesheni hii."
Wakati wa operesheni hiyo, magari saba ya al‐Shabaab na ugavi wa usafirishaji wa watu na vifaa viliharibiwa wakati silaha nyingine za namna mbalimbali na risasi zilipatikana, AMISOM ilisema. Siku ya Jumamosi, msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Kenya (KDF) Meja Emmanuel Chirchir alisema kwenye mtandao wa Twitter kuwa askari watano wa KDF walikuwa wamepotea kwenye tukio hilo, na watatu walipelekwa kwa ndege huko Dobley kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kupata majeraha. Baadaye watatu waliokuwa wamepotea walipatikana Jumapili, Chirchir alisema kwenye Twitter," Hongera vikosi maalumu na kwa ushindi wenu wa kishujaa"
Al-Shabaab iliweka picha za marehemu kwenye mtandao wake wa Twitter wakisema kuwa ni miili ya askari wanne wa KDF waliouawa katika mapambano hayo. Mashuhuda wa huko Kismayo walisema al-Shabaab ilileta miili hiyo kwenye mji wa bandari wakati wa usiku na kutoa wito kwa wakazi kutoka nje kuja kuwaona.
"Tuliona miili ya wanaume wanne wakiwa katika sare walioonyeshwa na al-Shabaab huko Kismayo," mkaazi wa eneo hilo Hassan Abdi Mohamud aliiambia AFP kwa simu. Alidai kuwa wawili kati ya waliokufa walikuwa askari wa Somalia na wawili ni Wakenya.
Miili hiyo bado haijatambuliwa na idadi ya waliokufa haijaweza kuthibitishwa na upande huru.
Somalia na vikosi shirika vinakusudia kuiteka Kismayo hivi karibuni , Maofisa wa jeshi walisema.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII