HAWA NDO WASIMAMIZI WA KAZI ZOTE ZA DIAMOND PLATNUMZ


  Mkurugenzi wa kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed akibadilishana mkataba na Msanii Diamond Platnumz baada ya kusaini. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo  na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole.

 Mkurugenzi wa Kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed ( kushoto)  na msanii Diamond Platnumz wakisaini mkataba  wa kufanya kazi pamoja. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo  na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole


MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameingia mkataba na kampuni ya I-View Studios ya ili wasimamie kazi zote kwa muda wa miaka miwili.
Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solution ya mjini Dar es Salaam, Petter Mwendapole amesema I-View itasimamia mikataba yote ya kazi zote za msanii huyo na yeyote atakayetaka kufanya kazi na Diamond kwa sasa itabidi awasiliane I-View.

“Diamond ameamua kufanya kazi zake kimataifa, na ameingia mkataba na I-View ambapo wao ndio watakuwa wakisimamia maonyesho, matangazo, nyimbo kwenye simu, nguo kila kitu ambacho kinahusiana nay eye kinapaswa kupitia I-View,” amesema.
Mwendapole alisema pamoja na maonyesho, lakini I-View pia itawajibika katika muonekano mpya wa msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba ndani na nje ya Tanzania. One Touch Solutions ndio watakuwa wasemaji wa msanii huyo. Diamond kwa upande wake alisema anataka kufungua ukurasa upya katika tasnia ya muziki nchini na kwa anaamini utasaidia katika kumfanya aongeze nguvu zaidi katika kutunga na kutengeneza nyimbo zake.

“Hii yote ni kuhakikisha nafanya kazi zangu kwa ufanisi badala ya kujirundikia mambo mengi, kuna watu walikuwa wakinitafuta wanashindwa kunipata lakini sasa watakuwa wanafahamu ofisi ziko wapi na wanawasiliana na menejimenti inawapa majibu, watu wa habari watakuwa na mtu wa kuwasiliana nae moja kwa moja hata kama sipatikani,” amesema.
Diamond anatarajia kutoa wimbo wake mpya ambao pia utarekodiwa na kampuni ya I-View. Tayari usaili umeshafanuyika kwa ajili ya wale ambao wataonekana kwenye video hiyo. I-View mbali na kazi kupiga picha, lakini pia inatengeneza matangazo mbalimbali ya TV, Radio, mabango, ubunifu wa kazi mbalimbali za sanaa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs