Wassira amtaka Dr. Slaa aache kuita wake za watu chumbani!

BongoNewz
Katika kile sasa kinachoonekana kuwa bifu kali kati ya hawa wanasiasa waili wa umri mkubwa, Waziri Wassira amemtaka Dr Slaa awe mwangalifu katka kutoa kadi za chama chake chumbani bila wadau wengine kuwapo!!

Kulingana na gazeti la Majira la tarehe 1/10/2012, Wassira alikuwa akijibu mapigo kwa jina lake kutumiwa na Dr Slaa katika kuwapa kadi wanachama waili wenye jina la Wassira.
Hata hivyo Nd Wassira alisema ndugu zake hao ambao ni watoto wa kaka yake,Lilian na Ester Wassira wana haki ya kujiunga na chama chochote cha kisiasa.
" Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Bunda,mkoani Mara, Bw Wassira alimshukia Dr Slaana kumtaka awe makini kuwaita wake za watu chumbanina kuwapa kadi bila maofisa wengine wa chama hicho kushuhudia tukio hilo."

Wassira aliendelea,
"Namtahadharisha Dkt Slaa kwani alichokifanya kinaweza kuleta mtafaruku katika ndoa za watu"

Maoni yako Kuhusu Kauli hii ya Mtu mzima please..
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

2 comments:

  1. Suala hilo linahitaji hekima , busara na utashi. Iwapo Dr. Slaa angekuwa na nia mbaya dhidi ya hao wanawake nafikiri yasingewekwa wazi kihivyo. Ila kikubwa kinachohitajika hapa ni busara na upembuzi yakinifu kwa haya yote yanayoendelea kujitokeza.

    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs