KAMBI YA LOWASA YAZIDI KUJIIMARISHA KUELEKEA 2015
BONGONEWZ BLOG
KAMBI ya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, imeendelea kuzidi kujiimarisha katika uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya wagombea wanaomuunga mkono kuzidi kupata ushindi.Katika chaguzi zilizokwishafanyika katika ngazi ya wilaya na mikoa, wagombea wengi wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Wazazi waliokuwa katika kambi nyingine ndani ya chama hicho wameshindwa.
Hata hivyo, katika uchaguzi wa UVCCM mkoa ambao ulifanyika jana katika mikoa kadhaa nchini inaonyesha kuwa kambi hiyo ya Lowassa inayoratibiwa na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa, Beno Malisa na Hussein Bashe wagombea wake wengi wameibuka na ushindi.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa Kambi ya Kada wa CCM, Bernard Membe ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi inaongozwa na Ridhwan Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Utekelezaji wa Baraza la Vijana wa chama hicho, ambaye kwa sasa amekuwa akipita mikoani kuongezea nguvu kambi yake.
Mkoani Arusha chaguzi hizo zilimalizika jana kwa wilaya nne za Mkoa wa Arusha, isipokuwa wilaya moja ya Longido, ambako uchaguzi unatarajiwa kurejewa katika nafasi ya NEC.
Katika Wilaya ya Ngorongoro, Mbunge wa jimbo hilo, Saning’o Ole Telele alitangazwa kuwa mshindi wa NEC baada ya kupata kura 457 dhidi ya Mathew Nasay ambaye alipata kura 323 na Ibrahim Sakayi kushinda nafasi ya mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo kwa kura 517 na kumbwaga aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Metui Ole Shaudo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji wa Ngorongoro.
SOURCE: MCL
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII