LEMA: "VIGOGO WA CCM MJIANDAE KUSTAAFIA JELA"....

Kwenye Exclusive interview aliyofanya na millardayo.com Godbless Lema (Chadema) alievuliwa ubunge wa Arusha mjini na Mahakama amekubali kutoa ya moyoni kuhusu vitu ambavyo chama cha Mapinduzi (CCM) kinakosea.

Naanza kumkariri akisema “kwanza ni uaminifu, vilevile ukishaona chama viongozi wake wanakosa vision kwa sababu hata katika maisha ya kawaida unafikia malengo kama una maono, muulize Waziri yeyote wa CCM ama kiongozi yeyote wa CCM, maono yao ya msingi ni ya kuweka CCM madarakani kwa gharama yoyote”

“Wajenge shule na waweke walimu wazuri ziwe na hadhi kama hizi English medium, wanasema wamefanikiwa wamejenga shule za kata, nionyeshe mtoto wa waziri mmoja anaesoma shule ya kata… jambo la msingi ambalo CCM wamelikosea sana ni kukosa vision, hakijui kinataka kuacomplish nini, kwa sababu kimekosa vision.. kimekosa teamwork yenye lengo moja, teamwork ya CCM ridhaa yao ni kushika power na sio kujenga maisha ya watu” – Lema

Alipoulizwa kuwa ni kiongozi gani wa CCM anaedhani ni mwema na anafaa kuhamia Chadema……. akajibu “wako watu, sio watu wote wabaya.. wako watu wanafiki, wezi na mafisadi, ushauri wangu kwa hao wazuri wanaofikiri wao wana wema wa kutosha wana nia nzuri na nchi yao, hii ni moment sasa ya kuja kuungana na jeshi lakini sio kama akina Sitta, hao wabaya ambao kwanza hata wakija hatuwapokei wasubiri jela tutakapochukua nchi, kuna watu watakwenda jela.. yani uzee wao kuna watu watastaafia jela kwa sababu wameifilisi nchi, CCM haiwezi kuwa na watu wote wabaya… wako wadogo wazuri lakini hao wakubwa hapo juu ndio wana shida”

SOURCE: MILLARD AYO
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs