Rais Kikwete atunukiwa Nishani ya Heshima na Sultani Qaboos wa Oman!!

BONGONEWZ BLOG


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwenyeji wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya AL Alam jijini Muscat Oman jana jioni muda mfupi kabla ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa kwa heshima yake.

 Sultani wa Oman,Qaboos bin Said Al Said akimtunuku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nishani ya juu ya heshima, Taifa la Oman wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake jana jioni katika kasri ya  AL Alam jijini Muscat Oman.
 Sultan Qaboos bin Said Al Said akimpongeza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku nishani ya juu ya heshima ya Taifa la Oman jana jioni katika kasri ya AL Alam. Jijini Muscat Oman jana jioni .Rais Kikwete aliwasili nchini Oman jana jioni kwa ziara rasmi ya siku nne.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs