KAMA WEWE NI SHABIKI WA SIMBA HII INAKUHUSU SAANA
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, wametenga kitita cha
dola 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 25) ili kipa wao, Juma Kaseja
aongeze mkataba.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa kipa huyo atatemwa Msimbazi baada ya
kuwasili kwa Abel Dhaira ambaye ni kipa namba moja wa timu ya taifa ya
Uganda.
Simba imegundua umuhimu wa Kaseja na imetangaza kumsainisha
mkataba mpya kwa kitita hicho, ikiwa ni siku chache baada ya kipa huyo
kutangaza kuwa yupo tayari kufanya mazungumzo na klabu yoyote.
Chanzo
cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya kamati ya usajili ya timu
hiyo, kimelithibitishia Championi Jumatatu kuwa kiasi hicho kimetengwa
kwa ajili ya kuhakikisha Kaseja anabaki Simba.
Chanzo hicho kilisema wanaheshimu uwezo wa kipa huyo, hivyo wameona ni vyema abaki kikosini ili asaidiane na Dhaira.
“Katika
kuhakikisha tunambakiza kipa wetu Kaseja, tayari tumemuandalia dola
20,000 ili aendelee kubaki kuichezea Simba msimu ujao.
“Tumeridhishwa
na kiwango chake ndani ya uwanja, tunaamini ni kipa bora mwenye uwezo
mkubwa golini, hivyo atabaki asaidiane na Dhaira,” kilisema chanzo
hicho.
Alipoulizwa ofisa habari wa timu hiyo kuhusiana na taarifa
hizo, alisema: “Muda wa usajili bado, ni vyema tukasubiri kwanza, kila
kitu tutakiweka wazi usajili ukifunguliwa.”
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII