"BABA HATAKI NIVAE NUSU UCHI, NA MIMI SIWEZI KUVAA GAUNI UTADHANI NIKO KANISANI"....LINAH

BongoNewz
  Mwimbaji Linah ambae juzi alitangaza  kwamba ameamua kuwazawadia wazazi wake nyumba aliyoijenga Mpiji Mbezi Dar es salaam kwa thamani ya milioni 30 za kitanzania, amesema pamoja na wazazi wake kufahamu kwamba matunda hayo yametokana na muziki peke yake, amekubali kwamba baba yake mzazi mpaka sasa bado hakubaliani na mavazi anayoyavaa Linah.

Namkariri Linah akisema “nimejitahidi sana kuwaelezea wazazi wangu wanielewe litakapotokea tatizo lolote itakua ni bahati mbaya tu lakini sio kwa makusudi, baba anaona pia kwenye magazeti huwa navaa hivi najitahidi kumwambia hivyo ni vitu vya bahati mbaya huwa vinatokea na mimi kama msanii ndio maana tunakula tunaishi lakini ndio kazi

Mbali  na hayo Linah kasema “nyimbo zangu baba anazisikiliza na anazipenda na anakubali ninaimba kitu ambacho kipo, ila ubishi mkubwa kati yangu na yeye ni mavazi, kuna show na show.. siwezi kwenda kufanya show ufukweni alafu nimevaa magauni, show nyingine tunatakiwa kubang siwezi kuvaa migauni kama niko kanisani”

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

2 comments:

  1. mi nadhani ni umasikini wa fikra tu na kushindwa kutambua thamani yake

    ReplyDelete
  2. Exactly Prince George, what I believe umaarufu hauji kwa kuvaa nusu uchi....kama mtu anapata umaarufu wa namna hiyo basi ndo ile tunaita 'CHEAP POPULARITY'

    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs