Bundi wavamia mkutano wa CCM!!!

BongoNewz
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, bundi wawili juzi walivamia mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya KAHAMA na nusura waangukie meza waliyokuwa wameketi Mbunge wa Kahama Mjini, James Lembeli na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja.

Kuingia kwa bundi hao katika uchaguzi uliokuwa unasubiri kwa hamu na wakazi wa Kahama kwenye Ukumbi wa Shule ya Msingi Rocken mjini hapa kuliibua hofu kubwa kwa wagombea, kiasi cha baadhi ya wanaCCM kugeuza tukio hilo kuwa ajenda kwa muda.“Ni ajabu kwa bundi kuingia katika ukumbi wa mkutano, hawakuogopa kelele za watu cha ajabu ni kutaka kuangukia meza za viongozi. Ni tukio la kustaajabisha sana,” alisema Damas Joseph, Diwani wa Kata ya Chambo wilayani Kahama.

Aliongeza kuwa, kama tukio hilo lina aina yoyote ya nguvu za giza, linapaswa kukemewa kwa nguvu zote kichama, kwa kuwa viongozi wa kweli wanapaswa kuchaguliwa bila `kuchezea’ akili za wajumbe ambao ni wapigakura.

MwanaCCM mwingine, Deo Ndilima kutoka Kata ya Ukune, alikiri kufadhaishwa na tukio hilo, huku akielezea hofu ya kutopatikana kwa viongozi wasio na sifa kukiongoza chama, hasa endapo bundi hao wanahusishwa na masuala ya ushirikina.

Ukiondoa tukio hilo, wajumbe wengi walisifu hali ya utulivu iliyokuwa inaendelea katika uchaguzi huo.

SOURCE: JF

 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs