CHADEMA yamuumbua mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
BongoNewz
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuonyesha ukomavu wa hali ya juu kimemjibu mkuu wa mkoa Bwana Gamma katika mkutano ambao haujaonekana mkoani Kilimanjaro baada ya uchaguzi mkuu kwa kueleza kinaga ubaga kuhusu ziara ya madiwani kwenda mafunzoni nchini Rwanda.
Akitoa ufafanuzi hatua kwa hatua huku akishangiliwa na umati wa wananchi meya wa manispaa ya moshi MICHAEL JAFFARY alimtuhumu mkuu wa mkoa kwa unafiki na kufanya mambo aliyotumwa na CCM ili kuiharibu na kuichonganisha na wananchi CHADEMA mkoani huko,alimhakikishia mkuu wa mkoa kuwa hakuna ufisadi kwa kuwa safari yote inajulikana ofisi ya waziri mkuu,mkuu wa mkoa mwenyewe na kuwa haitafutwa na iko palepale. Akafafanua kuwa hizo ni hasira za kufichuliwa ufisadi mkubwa katika miradi ya mabango ambapo manispaa ilikuwa inapata mil 70 nyingine zinaingia mifukoni mwa mafisadi,baada ya kuwabana sasa hivi mabango yanaingiza 400mil.
Akawataka UVCCM kuandamana kwa ufisadi mkubwa unaofanywa na serikali yao kwa rais kukaa hoteli za dola 10000 na timu za watu 20 na zaidi. Amewahakikishia wana Kilimanjaro kuwa CDM haiwezi kuwasaliti na kamwe wasidanganywe na CCM. Walifanya ziara Japan kwa kodi za walipa kodi wa Japan na sasa imefikia mahali manispaa imeamua kwa makusudi ya maendeleo na usafi wa mji wa Moshi kwenda kujifunza kwa wenzao. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuonyesha ukomavu wa hali ya juu kimemjibu mkuu wa mkoa Bwana Gamma katika mkutano ambao haujaonekana mkoani Kilimanjaro baada ya uchaguzi mkuu kwa kueleza kinaga ubaga kuhusu ziara ya madiwani kwenda mafunzoni nchini Rwanda.
Akitoa ufafanuzi hatua kwa hatua huku akishangiliwa na umati wa wananchi meya wa manispaa ya moshi MICHAEL JAFFARY alimtuhumu mkuu wa mkoa kwa unafiki na kufanya mambo aliyotumwa na CCM ili kuiharibu na kuichonganisha na wananchi CHADEMA mkoani huko,alimhakikishia mkuu wa mkoa kuwa hakuna ufisadi kwa kuwa safari yote inajulikana ofisi ya waziri mkuu,mkuu wa mkoa mwenyewe na kuwa haitafutwa na iko palepale. Akafafanua kuwa hizo ni hasira za kufichuliwa ufisadi mkubwa katika miradi ya mabango ambapo manispaa ilikuwa inapata mil 70 nyingine zinaingia mifukoni mwa mafisadi,baada ya kuwabana sasa hivi mabango yanaingiza 400mil.
Akawataka UVCCM kuandamana kwa ufisadi mkubwa unaofanywa na serikali yao kwa rais kukaa hoteli za dola 10000 na timu za watu 20 na zaidi. Amewahakikishia wana Kilimanjaro kuwa CDM haiwezi kuwasaliti na kamwe wasidanganywe na CCM. Walifanya ziara Japan kwa kodi za walipa kodi wa Japan na sasa imefikia mahali manispaa imeamua kwa makusudi ya maendeleo na usafi wa mji wa Moshi kwenda kujifunza kwa wenzao.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII