Msanii PIPI ajifungua Mtoto wa Kiume...
Nyota wa kizazi kipya hapa Tanzania namzungumzia Doreen Lucas a.k.a pipi ambaye amefanya ngoma kadhaa na wasanii mbalimbali hapa bongo land kama ile ya nikki wa pili ambayo ilikuwa inafahamika kwa jina la kiujamaa na zinginezo.Sasa habari nzuri ni kwamba msanii huyu kwa siku ya jana alifanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume na kumpa jina la Kingston.Msanii huyu baada ya kujifungua mtoto huyo wa kiume alifunguka na kusema kwamba anamshukuru mwenyezi mungu kwa kuwa mama wa mtoto kwani ni wangapi hivi sasa hawana watoto lakini mimi mungu amenipatia mtoto wa kiume na nimempatia jina la kingston.Hayo ndiyo maneno ya Doreen Lucas a.k.a pipi baada ya kujifungua mtoto wa kiume.
Source: DJFETTY TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Source: DJFETTY
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII