Mwandishi wa Habari wa Channel Ten afariki wakati Polisi wakitawanya Wafuasi wa CHADEMA Iringa


Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo. Vurugu hizo zilizopelekea kifo cha Mwangosi zilitokea katika kiwanja cha Mwembe Togwa baada ya polosi kuutawanya umati wa wafuasi wa CHADEMA waliokuwa kwenye mkutano katika uwanja huo.

Awali, polisi wilayani humo waliruhusu mkutano huo kufanyika katika uwanja huo na baada ya mkutano huo kuanza polisi waliuzuia na kuutaka uongozi wa CHADEMA kufanya mkutano huo baada ya Shughuli ya sensa kukamilika. Baada ya polisi kuona mkutano huo unaendelea waliamua kuutawanya mkutano huo kwa mabomu ya kutoa machozi na risasi za moto kitendo ambacho kilipelekea umauti kumkuta Bw. Daudi Mwangosi.

Mungu Ailaze mahali pema roho ya Daudi Mwangosi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs