Serikali ya Tanzania yaongeza muda wa mwisho wa sensa


Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) imetangaza nyongeza ya wiki moja ya siku ya mwisho ya sensa ya kitaifa. Sensa ilipangwa kumalizika Jumapili, wakati ambapo NBS ilisema asilimia 95 ya Watanzania walikuwa wamehesabiwa. Baadhi ya watu katika maeneo yenye ugumu wa kufikika walikuwa bado hawajahesabiwa, ambao muda wa mwisho uliyoongezwa unakusudia kuwafikia.

NBS ilikabiliwa na changamoto za awali katika kukusanya data kwa ajili ya sensa, ikiwa ni pamoja na upungufu wa sare kwa ajili ya maafisa wa sensa na upungufu wa fomu za sensa.

"Katika makao makuu, tuliweka pamoja mfumo mzuri wa usambazaji, lakini baadhi hawakuufuata. Hivyo, vifaa kwa ajili ya mahali fulani vilipelekwa mahali pengine -- hii ndiyo sababu baadhi ya sehemu hazikuwa na fomu za kutosha," alisema ofisa wa habari na uhamasishaji wa NBS Said Ameir.

Tangu wakati huo ofisi imeanzisha mfumo wa miadi na namba ya simu ya moja kwa moja ya sensa, ambapo Watanzania wanaweza kupanga miadi na wawakilishi wa sensa kwa kupiga simu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs