MADAM RITA AELEZEA JINSI ALIVYOPATA MIMBA AKIWA NA MIAKA 14, SOMA HAPA
Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen aka Madam Rita
amesema yeye ni miongoni mwa wanawake waliopata ujauzito wakiwa na umri
mdogo lakini alikuwa jasiri wa kukabiliana na hali hiyo hadi
akafanikiwa.
Kupitia Facebook, Madam Rita amewashauri wasichana wanaojikuta katika
katika hali hiyo kutokata tamaa kwakuwa bado wanaweza kufanikiwa.
“Jambo moja msilofahamu kuhusu mimi,Nilipata ujauzito nikiwa na umri
mdogo sana. Kwa jamii yetu inayotuzunguka, ukizaa katika umri mdogo,
watu huwa wanakunyanyapaa, hukuona haufai kuwa katika jamii na hata
kukuhukumu.
"Kwa umri ule niliona ni kama hamna tena maisha kwangu lakini
sikukata tamaa na leo hii ujasiri wangu na kitu kinachonipa msukumo wa
maisha hadi kufika hapa nilipo ni hicho kilichonikuta nikiwa na umri
mdogo.Kukataa tamaa isiwe ndio chaguo lako la kwanza,” aliandika Rita.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII