UNAMKUMBUKA BABY J?? BOFYA HAPA KUSOMA UNDANI WA MAISHA YAKE


Baby J.
ANAOMBA UCHUMBA

Baby J nakuzimia sana kwa uimbaji wako mzuri kunako gemu la muziki wa kizazi kipya Bongo, je, umeolewa? Nataka uwe mchumba wangu. Salim Liundi, Dar, 0658110395

BABY J: Asante, tayari nimeolewa.
NDOA, WATOTO

Binafsi nakukubali sana Baby J ila nataka kufahamu una muda gani kwenye ndoa na je, una watoto wangapi? Amiri Salumu, Dar, 0653252416

BABY J: Ndoa yangu ina miaka miwili sasa bado sijapata watoto.
ANAISHI ZANZIBAR?

Baby J nini kilichokuvutia kuishi Zanzibar? Umeolewa? Patrick…
Baby J.
ANAOMBA UCHUMBA
Baby J nakuzimia sana kwa uimbaji wako mzuri kunako gemu la muziki wa kizazi kipya Bongo, je, umeolewa? Nataka uwe mchumba wangu. Salim Liundi, Dar, 0658110395
BABY J: Asante, tayari nimeolewa.
NDOA, WATOTO
Binafsi nakukubali sana Baby J ila nataka kufahamu una muda gani kwenye ndoa na je, una watoto wangapi? Amiri Salumu, Dar, 0653252416
BABY J: Ndoa yangu ina miaka miwili sasa bado sijapata watoto.
ANAISHI ZANZIBAR?
Baby J nini kilichokuvutia kuishi Zanzibar? Umeolewa? Patrick Mlonge, Morogoro, 0789371830
BABY J: Zanzibar ndiyo nyumbani kwetu na nimeolewa.
MAVAZI
Baby J wewe ni dini gani kama Muislamu kwa nini usivae nguo za heshima kuliko unavyovaa suruali? Kwa nini usilete utofauti wa mavazi kwa wasanii wa kike wa bara na visiwani? Salehe Suleimani, Dar, 0717416248
BABY J: Mimi ni Muislamu, mavazi hayajalishi dini ya mtu ila nitaufanyia kazi ushauri wako.
DAR NA ZANZIBAR
Baby J ni nini kilichokufanya uhamie Dar kufanya muziki? Je, Zanzibar hakuna soko? Abdallah Ramadhani, Dar, 0717060706
BABY J: Mimi ninaishi Zanzibar na muziki nafanya huku sijawahi kufanyia kazi Dar.
KIMYA
Dada mbona sasa upo kimya au maisha ya ndoa yanakufanya usisikike na kitu kipya? Rama Nuru, Dar, 0682885844
BABY J: Niliamua kukaa kimya kwa muda kwa sababu kuna mambo binafsi nilikuwa nafanya, ndoa haihusiani kabisa na kazi yangu.
ANAMFAHAMU
Ninavyokujua Baby J kwenu ni Kiembe-Samaki, Zanzibar, umesoma High View na mtihani wako wa kidato cha nne ulipata ziro kwa sababu usiku wa Jumapili ulifanya shoo pamoja na Dogo Mfaume na Berry Black Bwawani na asubuhi yake ulikuwa unafanya mtihani wako wa mwanzo. Je, unaweza kukataa? Ommy, Zanzibar, 0715655819
BABY J: Ni kweli.
YEYE NA DIAMOND
Baby J kuna tetesi kwamba unataka kufanya kazi na Diamond (Nasibu Abdul) je, ni kweli? Msomaji, 0718837841
BABY J: Nina mpango huo.
NDUGU
Baby J wewe ni msanii wa muziki, baadhi ya wasanii wana tabia ya kujisikia na kutojali ndugu zao, je, wewe ni mmoja wao? Johnson, Muheza, 0684779575
BABY J: Hapana, ninawajali sana ndugu zangu hata watu wengine pia.
AMEACHANA NA MUMEWE?
Kiukweli nakukubali sana Baby J, mtoto wa Bi Mode, eti ni kweli umeachana na mumeo? Mary, Zanzibar, 0654155359
BABY J: Mume wangu niko naye na ninampenda sana.
MUMEWE NI MSANII?
Nakupenda sana Baby J vipi mumeo naye ni msanii na kama siyo anafanya kazi gani? Tuma, Mbeya, 0768631366
BABY J: Siyo msanii ni mfanyabiashara.
MUMEWE AMEFUNGWA?
Eti mume wako amefungwa pande za Ulaya? Msomaji, 0715306567
BABY J: Hapana hayo ni maneno ya watu tu.
ANARINGA?
Ninavyokujua mimi unaringa sana hata kwa mashabiki wako Baby J. Kwa nini? J, Dar, 0717096803
BABY J: Mimi siringi nadhani wewe hunifahamu vizuri kwa sababu mimi naongea na kila mtu sichagui wala sibagui.
WATOTO
Baby J wewe ni mkali katika gemu la muziki na ninakukubali, napenda kujua una watoto wangapi? Johari, Mwanza, 0753084572
BABY J: Nashukuru sana, sina watoto.
YEYE NA WOLPER
Eti Baby J una undugu na Wolper (Jacqueline) na ningependa tufanye kazi wote nina kipaji dada. Cherly, Dar, 0653956467
BABY J: Hapana siyo ndugu yangu ila ni rafiki yangu sana, kuhusu kufanya kazi hamna shida tutafanya tu.
RUSHWA YA NGONO
Baby J kuna tetesi kuwa wakati ulipotaka kujiunga na muziki kuna prodyuza mmoja alikuomba rushwa ya ngono, vipi kuhusu hilo? Issa Chongono, Tanga, 0714455748
BABY J: Kwa msanii kuombwa rushwa ya mapenzi ni vitu vya kawaida kwani ni jambo linalotokea mara nyingi sana ila ni akili tu ya mtu.
NDUMBA
Dada nakupongeza kwa kazi nzuri ila nasikia mtaani wanasema unatumia ndumba kwenye mapenzi ndiyo maana Mkenya amedata kwako, ni kweli? Seleman, Mbezi, 0654825568
BABY J: Siyo kweli na mume wangu siyo Mkenya ni Mzanzibar lakini amekulia Marekani.
SOURCE : GPL
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs